Yaweza Kuwa Sababu Kubwa Kufeli Kwa Online Marketing Africa?

KijanaHuru

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Posts
1,822
Reaction score
2,320
Habar wana jamii wenzangu,
Ninalolileta halijawekewa takwimu na vyombo vinavyojishugulisha na utafiti,
Lakini ni maono yangu binafsi tu yanayofanya nione kama hivi.
Jambo la kwanza lililofanya mpaka nianze kutafuta sababu haswa ni mara pale nilipoona jinsi ambavyo online marketing zikifeli vibaya sana kufanya kazi hapa Africa.
Haswa ie zinazojumuisha Peer To Peer kama GNLD,Forever Living,Universal,Four Corners,Helping Hands, Na zingine kibao zenye Mifumo hii.
Kwanini nasema hazijafanikiwa?
Hazijafanikiwa kwasababu moja kubwa hii wengi wa ambao wanajishugulisha na hizi mambo, ni bado wako vilevile na zaidi tunawaona jinsi ambavyo wanazidi kudidimia kiuchumi huku wakizidi kujifariji kwa ndoto za alinacha za kuwa mamilionea kwa gafla kupitia hizi biashara.
Mimi nilikuwa ni mmojawapo niliye jiunga na hizi biashara na kuzifanya baadhi
Kama
-Four Corners Alliance Group
-Helping Hands
-Crowd Rising
-Universal plan B
Mimi kwa wanachama wenzangu nilikuwa naonekana jembe sababu nikaonekana ndiye mchapakazi haswaaa ila mwisho wa siku nikajiona kuwa mburula kuzidi hata wale mburula niliokuwa nawaona.
Sasa nakuja kwenye Point yangu iliyofanya niweze kujiuliza hili swali
Yaweza Kuwa Sababu Kubwa Kufeli Kwa Online Marketing Africa?
Naanza kwa kurudi miaka mingi sana nyuma Africa kabla hatujaanza kuendelea tukiwa na tamaduni zetu na U-arica wetu halisia Hata kabla akili haijaamka sawa tukawa katika mikono ya watu wengine tukigeuzwa kama nyanya za kuuzwa na maroboti ya kufanya kazi(Utumwa na Ukoloni)
HIi hali ilitufanya tujue yakuwa mwenye nguvu ndiye anayeishi na mwenye nguvu ndiye anaye amua,
Tukiwa bado katika hali ya hasira ya kuonewa na kutumikishwa basi tukapigwa na msumari mmoja wa dini, hapo wakawa wamemaliza kila kitu juu ya akili na mawazo yetu pamoja na misimamo yetu.
Akili zetu zinaendela kufunguka lakini tukiwa mikononi mwa watu, wao wamezifungua kwa namna yao wao wenyewe.
Sasa hadi tunapokuja kupata uhuru na kuanza kujitegemea kuna makovu ya kisaikolojia tunakuwa tumeachiwa.
Mfano Tunaamini lazima utoke jasho uweze kupata faida(Kama tulivyotawaliwa)
Na ni kama roho inayojirithisha kizazi hata kizazi
Sasa leo mwafrica unamletea hadithi za kununua madawa na awe milionea daaaaaaa?
Inakuwa vigumu mno maana hizi biashara zinahitaji akili zaidi kuliko nguvu.
Nasisi tunajua nguvu zaidi kuliko akili ila ukipata ndio tumia kwa akili(Japo si wote wachache wamekomboka)
Kwahiyo ni kama hivyo, mtu anaweza akawa na elimu kubwa ya juu sana lakini mwisho wake hawezi hata kujiokoa ajijengee mazinginra ya kujiari yeye mwenyewe
Bali atafanya kazi maisha yake yote akitegemea pensheni tu.
Wengin tumeona mda wa kazi unaisha anatakiwa atoke nyumba ya kampuni na hana hata kwakwenda,(Bado Mtumwa kifikra)
sasa hata hizi mambo za online business zinashindwa kwasababu zinahitaji akili zaidi kuliko nguvu na sivyo akili zetu zilivyo.

NB:Zipo baadhi zinafanikiwa na wapo baadhi wanafanikiwa, Ila ukifanya utafiti kuna kitu cha ziada kinakuwa kinafanyika tofauti na wengine
 
USISEME BIASHARA ZA NETWORK AFRIKA ZINA SHINDWA,SEMA TANZANIA NA SI KWA WATANZANIA WOTE,WATANZANIA WANAO JITAMBUA,WAMEFANIKIWA SANA,TENA HUMU HUMU TANZANIA.UKIENDA KENYA,UGANDA,ZAMBIA,MALAWI,MSUMBIJI,LESOTHO,ZIMBABWE,AFRIKA YA KUSINI ,WATI WANA FANIKIWA KWENYE HIZI BIASHARA.
TATIZO WATANZANIA WANATAKA WAANZE LEO NA KUPATA LEO,AKIAMBIWA AANZE KUJIFUNZA NA KUFANIKISHA ANAONA AMEIBIWA,YEYE ANATAKA AKIINGIA TU HATA KAMA HAJAFANYA KAZI YOYOTE AANZE ,SASA HIYO NI AKILI YA AINA GANI?
LAKINI PIA HATUPENDI KUJISOMEA LAKINI NI WABISHI NA WAJUAJI.
MTU AKAWEKA TANGAZO LA FURSA YA BIASHARA,UNAKUTA MTU ANAANZA KUKASHIFU NA KUTUKANA KABLA HATA HAJA CHUNGUZA,HAJAJIFUNZA NA KUELEWA
MIMI NASEMA BIASHARA YA MTANDAO NDIO FURSA PEKEE YA KUONDOA UMASKINI
,KWA SABABU NI BIASHARA YA KUSHIRIKIANA , WAVIVU WA KUJIFUNZA WATAKASHIFU,WATATUKANA LAKINI IPO WATAKUBALI.
BIASHARA YA MTANDAO NI BIASHARA YA KIMATAIFA
MASHARTI NI RAHISI INGIZA WATU WANNE CHINI,NA SIO WATANZANIA TU,ILA MTU WA NCHI YOYOTE,SIWEZI KUKOSA WATU WANNE TANZANIA ILA LABDA NI MVIVU NA MKATA TAMAA
UNAPOITA BIASHARA YA MTANDAO NI UTAPELI WAKATI INA OFISI INA VIBALI NA IMESAJILIWA,HATA KAMA SIO HAPA NCHINI,LAKINU IMESAJILIWA ILIPO TOKA UNA MAANISHA NINI? HIVI UNAJUA KUNA KUONGEA NA KUROPOKA
MIMI NINA IAMINI BIASHARA HII,WASIO TAKA KUJIFUNZA HAWATA KAA WAIAMINI,MAANA DUNIANI KUNA AINA 3 ZA WATU
1.WANAO SABABISHA VITU KUTOKEA
2.WANAO TAZAMA VITU VINAVYO TOKEA
3.WANAO ZUNGUMZIA VITU VINAVYO TOKEA
Hawa wazungumzaji ni balaa,maana wanazungumza vitu ambavyo hata hawajawahi kuvijaribu wala kuvifanya,wanajifanya wanajua wakati hawajui lolote,na ndio wengi huku kwetu.
 
soma elewa hoja sio unasoma kwa kujua hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…