MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,143
Habari wana JF,
Leo nimeanza kuamini kuwa wale jamaa wa TUMA KWA NAMBA HII ni matapeli walio kwenye ama makamouni ya simu ama mabenki yetu.
Leo nimetumiwa kiasi fulani cha fedha kwenye simu yangu. Aliyenitumia ametumia bank kuja kwenye mtandao wa simu.
Kabla hata sijamaliza kusoma ujumbe wa muamala huo zikaingia meseji tatu tofauti zote zikitaka kunitapeli kwa kunielekeza kuwa ile tuma kwenye namba hii.
Waliwezaje kujua kama kuna muamala simu yangu imeuapata kama sio organized crime?
Cha kushangaza nilikuwa na kama miezi mitatu siitumii simu yangu kwenye miamala lakini ghafla tu nimeanza kuitumia tayari na matapeli nao wameniona kuwa kiasi cha fedha kimeingia.
Tuishi kwa tahadhali kubwa enzi hizi za wizi wa mtandao. Tusitume fedha ovyo kwa watu tusiowajua na ikiwezekana mpigie simu mtu kabla ya kumtumia fedha ili kijiridhisha kama kweli ni mlengwa.