Yaya Toure atwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika

Yaya Toure atwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
1.8487814.jpg

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Toure alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika inayotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Yaya Toureamefanikiwa kuibuka na ushindii wa baada ya kupata kura nyingi zaidi ya Pierre-EmerickAubameyang, Andre Ayew, Yacine Brahimi na Sadio Mane.
86610826_afoty-2015.jpg

List ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa BBC

Kutwaa tuzo hiyo kwa Yaya Toure kunamfanya kuwa mchezaji wa tatu kuingia katika rekodi ya wachezaji wa zamani wa Nigeria Nwankwo Kanu na Jay-Jay Okocha ambaoo kila mmoja katwaa tuzo hiyo mara mbili, rekodi ambayo inashikiliwa na wachezaji watatu kwa sasa ikiwemo Toure.

e.jpg

List ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo hiyo

Toure kwa mara ya kwanza alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBCmwaka 2013, baada ya ushindi wa tuzo hiyo hii ni moja kati ya sentensi za Yaya Toure ?Najivunia kupokea tuzo hii kutoka kwa mashabiki wangu siwezi kuamini?

Chanzo: Mitandaoni
 
Wanapendelea hao, ilikuwa ya SAMATA hii
 
Amestahili Sana na Jana kadhihirisha yeye Ni bora afrika kwenye game Watford vs man city
 
Back
Top Bottom