Yellow Card: Movie moja matata yenye mafunzo

Yellow Card: Movie moja matata yenye mafunzo

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
5,039
Reaction score
6,253
Kwema?
Yellow Card ni movie moja matata sana iliyotoka mwaka 2000, nyota mkuu katika movie hii ni kijana mtanashati "Leroy Gopal "wa Zimbabwe,
Director wa movie hii ni John Riber, Story ya movie namna ilivyo ni huyu kijana Leroy kua na ndoto za kucheza mpira nje ya mipaka ya nchi yake yaan Zimbabwe,
Tena kipindi hicho kijana alifananishwa na nguli wa soka duniani Ronaldo Luis Nazario de Lima "The phenomenon ", pamoja na kua na ndoto kubwa ya kucheza soka lakini kijana aliendekeza ngono tena akiwa shule kiasi kilichopelekea kumpa mimba binti wa shule,
Binti baada ya kujifungua alimpeleka mtoto kwa mshikaji, basi jamaa akienda mazoenzi anabeba mtoto wake mgongoni anapiga soka...

Movie hii nilipata kuiona kwa jirani yetu mtaan maana peke yake alikua ana Tv , kama kawaida ITV waliwakilisha tena wao walitafsiri kwa kiswahili
Pia kijana alikua na rafiki yake alipenda sana ngono mwisho wa siku alipata magonjwa ya zinaa
Baadhi ya wahusika katika movie hii ni Leroy Gopal "Tiyane Tsumba", Ratidzo Mambo "Linda karombo, Collin Sibangani Dube "skido, ......
Screenshot_20190131-220351.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naikumbuka hii movie ya Tiane ... ili faulu sana kuweza kuziteka hisia za watu .... lakini mwisho wake haukiwahi kunivutia ... tulipaswa kujua hatima ya Tiane ilikuwa ni ipi katika kuipigania career yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani pale director alichemka maana tuliona jamaa anapata mwanamke ambaye kwao ni matajiri basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...Basi miaka yote najuaga ile picha ina part two mimi tu sijaiona, kumbe wengi tumeona tatizo lake.

Enzi za itv huku yellow card huku Neria.
 
Write your reply...Basi miaka yote najuaga ile picha ina part two mimi tu sijaiona, kumbe wengi tumeona tatizo lake.

Enzi za itv huku yellow card huku Neria.
Ni mapungufu yaliyopo katika ile movie hata ulaya pia hua wanakosea mda mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kale kajamaa kafupi si kalipata ukimwi?.. naskia ina part two hiyo movie
 
Kuna ile muvi inaitwa Tsotsi kutoka south basi mm nilikua najua hii ndo inaitwa hivo.. kumbe ni muvi 2 tofauti

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Nadhani pale director alichemka maana tuliona jamaa anapata mwanamke ambaye kwao ni matajiri basi

Sent using Jamii Forums mobile app
Haukuona maudhui yafuatayo
1) Mgongano wa matajiri na masikini
2) Ubaguzi wa ranging
3) maambukizi ya magonjwa ya ngono refer yule shabiki msela namba moja wa msela alipata gono na HIV
4) Hukuona ufuatiliaji wa vipaji refer kocha alivyokuwa anamfuatilia yule jamaa star ....acha niishie hapo kwanza.... Ukinijibu hili ntaendelea.... Inawezekana tunaangaliaga movie kwa angle gani
 
Vyote niliviona mkuu

Back
Top Bottom