Uchaguzi 2020 Yeremia Maganja: Tanzania ni nchi yenye maziwa na asali

Uchaguzi 2020 Yeremia Maganja: Tanzania ni nchi yenye maziwa na asali

NCCR Mageuzi

Member
Joined
Oct 3, 2007
Posts
23
Reaction score
63
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ndugu Yeremia Kulwa Maganja, jana Jumatano Septemba 30, 2020, alifanya mkutano kwenye Jimbo la Kigoma Kaskazini viwanja vya Bitale Sokoni kwa lengo la kuomba kura pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini ndugu Kitentya Luth.

Akiongea na umma wa wana kigoma Kaskazini Mgombea Urais ndugu Yeremia Kulwa Maganja amesema nchi hii kama ingekuwa inaongozwa vizuri tangu uhuru basi ingekuwa ni ujerumani ya Afrika kwa sababu Tanzania ni nchi yenye maziwa na asali.

Ameeleza pia kuna shida kubwa ya namna tunavyoongozana na kutendeana kijamii, kisiasa pamoja na kiuchumi huku akieleza chanzo cha haya yote ni pamoja na utekelezaji wa azimio la Arusha ambao haukuzingatia mazingira ya watu wake.

Mbali na hayo mgombea Urais ndugu Yeremia Kulwa Maganja hakusita kueleza vipaumbele vya serikali atakayoiongoza ya NCCR-Mageuzi pindi watakapompatia kura akitumia Ilani pendwa ya chama cha NCCR-Mageuzi.

Leo Oktoba 01, 2020 Mgombea Urais ndugu Yeremia Kulwa Maganja anatarajiwa kuwepo kwenye viwanja vya Mwanga Sokoni Jimbo la Kigoma Mjini akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo ndugu Wiston Andrew Mogha.

mj.png
 
Wanasiasa lopolopo tu
Atuoneshe mfano kwanza yeye alichofanya

Ova
 
Ni katika kampeni 😁😁
*Ila linaukweli ndani yake shida ni katika utekelezaji
*Sijui tunakwama wapi🤔
 
Back
Top Bottom