Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Unaweza kuishi na mtu Miaka nenda Rudi lakini usiujue uwezo wake.
Kimichezo, huwezi kujua uwezo wa mshambuliaji wa timu yenu zaidi ya Beki anayemkaba Mshambuliaji wenu.
Yaani Mabeki wa Barcelona hawawezi uelewa uwezo wa Messi uwanjani kuliko Mabeki wa timu zingine kama Real Madrid.
Huwezi Jua Msimamo na uwezo wa Mkeo au mumeo kukataa na tamaa yake zaidi ya wale wanaomtongoza Mumeo au Mkeo.
Yericko Nyerere na wenzake hawana uwezo wowote wa kuelezea uwezo wa Tundu Lisu.
Watu pekee wanaomjua Tundu Lisu uwezo wake namba Moja kabisa ni Hayati John pombe Magufuli na washauri wake wote.
Hao wanaweza wakakueleza Tundu Lisu ni mtu wa aina gani.
Kipindi cha awamu ya tano wakati nchi nzima ikiwa imetulizwa, ikatulia, uwanja ukiwa umeinama, wapinzani wakiwa hoi dhidi ya JPM na team yake.
Lisu ndiye aliyekuwa kinara yaani kama kwenye Filamu tungesema Mhusika Mkuu katika mapambano ya awamu ya tano walikuwa ni Lisu Vs JPM.
Na mechi ilichezwa dakika Mia na ishirini Mpaka Penati.
Lisu licha ya kushambuliwa vikali lakini hakujisalimisha,
Ilifika hatua nchi ikabaki na watu wawili tuu. Yaani JPM Vs Lisu.
Sisi wengine akiwemo Yericko na wenzake tulibaki mashimoni kama panya Buku, tukigeuka Keyboard warriors huku tukimwambia Maxence Melo asije akatuuza 😃😃
Usalama wa taifa, serikali ndio inajua uwezo wa Lisu kwa sababu wao ndio wanakuwa wanakinzana mara kwa mara. Lakini sio kina Yericko.
Kwa Sisi watunzi wa simulizi na filamu, Lisu tungempa uwezo wa ajabu na ikiwezekana kumnusuru kivyovyote ili mwisho Adui kuu akutane na Star.
Nishamaliza