NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
Ameandika Yericko Nyerere [emoji3578]
"Hii haikubaliki kabisa, mgawanyo huu wa mapato ni wizi wa mchana kweupe. Klabu mwenyeji wa mchezo haiwezekani ipate karibu chini ya 30% ya mapato. Hebu fikiria, Mchezo wa Simba vs Yanga wa jumapili 16/4/2023, kwa mujibu wa TFF uliingiza TSH. Million 410,645 000 halafu Klabu mwenyeji wa mchezo Simba kuambulia milion 188,898,504 tu.
Ukisoma kinachoitwa ni Mchanganuo wa Pesa ulivyo utaona ni wizi mtupu, Mfano; VAT ambayo kisheria ni 18% ambapo kwa TFF wamesema ni mil 62,640,762, inautata maana kisheria 18% hukatwa baada ya kutoa gharama uendeshaji, Tuwahoji TFF hii pesa waliyokata ni baada ya kutoa gharama za uendeshaji?. Sasa tuje, BMT imechukua million 10, 440,127. Hatujaambiwa kwa sheria ipi au kwa kanuni ipi ili tui challenge hiyo kanuni. Kisha tunaambiwa Uwanja wa Mkapa wao wamechukua million- 47,246,795. Bila kusema ni kwa kanuni ipi na wanatafsiri ipi kati BMT na Uwanja
Kisha tunaambiwa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limechukua million -12,599,145, Bila kuambiwa wamechukua kwa kanuni ipi inayowaelekeza kuchukua kiasia hicho. Halafu chombo cha TFF yaani mkono wa kulia wa TFF unaoitwa Bodi ya Ligi ukachota milioni 25,198,290. Sasa hapa unatofautishaje kati ya TFF na bodi ya Ligi ambacho ni chombo cha TFF?
Hawakuishia hapo, Kuna chama cha soka Mkoa kinachoitwa FA mkoa kikajichotea milioni 18,898,718 bila kuelezwa kwa sheria au kanuni ipi na kimehusikaje na mechi za Ligi Kuu Tanzania. Wakaja na Gharama za tiket, hawajaeleza wana maana gani kusema gharama ya tiketi, bila shaka ni kampuni zilizoprint na kuuza tiketi ambapo wamezilipa milioni 22,585,475.
Kituko kingine cha wizi wamekuja kuchota pesa milioni 22,048,504 kwakusema ni za "Gharama za mchezo", Unaweza kushangaa na roho yako! Sijui wana maana gani, Yaani gharama walizochukua TFF, Bodi ya Ligi, Uwanja wa Mkapa, BMT na FA Mkoa sio gharama za mchezo bali kuna kikundi kingine kinachojilipa kinachoitwa gharama ya mchezo?. Vyombo vyote vilivyochota pesa hapo juu ni vya serikali, ilitosha baada ya makato ya TRA, kinachofuata kiwe klabu mwenyeji kuchukua 70% ya kilichobaki baada ya kodi kisha TFF na wahuni wengine wote waliochota pesa hapo juu basi wagawane 30% iliyobaki.
Shirikisho la Mpira nchini TFF litoe maelezo utata wa makato haya, Vilabu vinatumia gharama kubwa sana katika kuandaa timu zao lakini pesa ikiingia zaidi ya 70% zinaliwa na magenge ya uhalifu yaliyojificha katika mpira nchini. Pengine tuombe ukaguzi maalumu wa CAG katika mechi hizi za watani wa jadi na ikiwezekana ufanyike ukaguzi wa jumla kuanzia BM hadi huku chini.