Yeriko Nyerere anachangia sana kuua demokrasia CHADEMA; amekuwa chachu ya kugawa watu hasa wanachama wanaopingana na mtizamo wake

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kila anayepingana na mtizamo wa Yeriko Nyerere anaonekana kama siyo mwadilifu na hana nia njema na chadema.

Yeriko anaamini anavyotambua yeye kampeni zilipaswa ziwe na elementi ya heshima kwa Mbowe. Anashindwa kutambua kwamba madaraka ya kisiasa siyo kubembelezana na kusifiana.

Hata Mbowe angekuwa na miemuko kama ya Yeriko sidhani kama CHADEMA ingekuwepo. Matusi na kutisha wanachama kuwaondoa kwenye kisa wamepingana na Mbowe siyo mfumo wa demokrasia. Siyo kila mtu ataweza na kutenda kama Yeriko. Baadhi wana fikra tofauti na lazima wasikilizwe.

Katika kipindi ambacho Yeriko ameonyesha kutokuwa na uvumilivu ni kipindi hiki. Siyo yeye tu bali hata akina Wangwe, Mbowe Jr, na Ntobi wameonyesha kutokomaa kisiasa na kutambua haki ya kugombea na kuchaguliwa inabaki kwa wapiga kura siyo wana mitandao.

Wagombanao ndio wapatanao.
 
Kuna watu wa kuwafuatilia.... Si hyo k uma
 
Nafikiri Mbowe ndiye anachangia kuua demokrasia kwani nyuma ya Yericko Nyerere yupo Mbowe. Haya yote yanayoendelea watu kuvuana nguo ni matokeo ya Mbowe kung'ang'ania madarakani. Baada tu ya Lissu kutangaza nia ya kugombea uenyekiti ndipo chawa wa Mbowe Yericko Nyerere, Boniyai na Ntobi wakaanza kumshambulia na kumtukana Lissu kwa kutumia haki yake ya kidemokrasia ndani ya Chadema kuomba kugombea uenyekiti. Na pia wapambe wa Mbowe wa mitandaoni wakiwepo wa JF wakamshambulia sana Lissu mashabulizi ambayo yalifungua milango kwa wafuasi wa Lissu nao kujibu mapigo na ndiyo hiki kinachoendelea hadi leo hii. Naamini kabisa 100% kama Mbowe angewakataza hawa wafuasi wake kumshambulia Lissu wangemsikia na mambo yangekuwa shwari lakini kwa vile alikuwa anawatuma na akiamini watamsaidia kumbe wanakivua nguo chama na kuipa CCM nondo za kuja kuichapia Chadema kwenye uchaguzi mkuu baadae mwaka huu. Kwa sakata hili lawama zote kwa Mbowe kwani alikuwa na uwezo kabisa wa kulizuia.
 
mbona pale Tanga aliwatuliza Wapenzi na wanachama kwenye Msiba. Mbowe anashindwa nini kuituliza hali kwa sasa. Kuna jambo
 
Back
Top Bottom