🚨Yes Mwaka 1991 ndo Mitsubishi RVR anazaliwa huko Japan

🚨Yes Mwaka 1991 ndo Mitsubishi RVR anazaliwa huko Japan

Samatime Magari

Senior Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
119
Reaction score
457
1729078039523.png
1729078062911.png

Ilipofika 2002 uzalishaji ukasimama wenyewe wanaita [production halt], Huu ni usimamishaji wa uzalishaji kutokana na kushuka kwa mauzo na kutopokea order mpya. Najua umejiuliza kwanini uzalishaji ulisimama, sababu Kwenye Biashara Kubwa mauzo yakianza kushuka na usipopokea order mpya [minimum order quantity] Kwa zaidi ya siku 180 basi ili hasara isiwe kubwa sana unapiga chini uzalishaji.

.
Hii ndo kitu iliowakuta RVR back in the days, unaweza jiuliza nini hasa kiliwakuta RVR kama RVR, Kwa kifupi tu Machine ilikua na mizinguo mingi kuanzia body, engine na vitu zingine. So 2002 wakaacha uzalishaji wakarudi kujipanga kwa miaka 8 na 2010 ndo Jamaa wakarudi tena wakaja na hii chuma ambayo kwa sasa inafanya vizuri..
.
Na hii ndiyo ninayoenda Kugusia in detail na kwa ufupi then utaona uishi nayo au lah, hii machine wameiterm kama Generation ya tatu Ya kwanza 1991-96, G2 1997-2002. Na gari ni mdogo wake Mitsubishi Outlander so wanashare components nyingi tu Na Japan ndo anaitwa RVR yani Recreation Vehicle Runner.
.
1729078249575.png
1729078258480.png
.
Nje ya Japana anaitwa Mitsubishi ASX, ASX ni kifupi cha Active Sport Crossover, Cross over ni gari ndumila kuwili [anagusa SUV same to gari za kawaida]. Speaking of body maboresho makubwa yalifanyika na lengo likiwa ni kupata SUV ndogo nje kubwa ndani. So wameipa simple Sport look ikiwa na muonekano very amaizing bongo zozo anasema fujo isiyoumiza..
.
Na ukiangalia iko chini halafu ni pana na fupi design inayoifanya kuwa na space kubwa ndani. Ukiingia ndani dashboard haina mambo mengi ina clusters zake mbili za speed na RPM. Kati kuna Digital display ikikupa taarifa za joto la engine na level ya mafuta Km + taarifa zingine.
.
Infotainment na control za ubaridi wameziposition vizuri usipate tabu kufanya setting wakati unaendesha. Leg room ni kubwa kama likes za SUV na zina upright seating position unaketi Kama unataka kupiga passport size sio the likes kama Rumion hivi, Maana kuna gari ukikaa utafikiri unataka kujifukiza.
.
1729078434233.png
1729078496222.png
.
Sema roof yake sio ndefu so kama wewe ni mrefu kuanzia kiunoni unaweza pata tabu kidogo mixer kugusa juu. Seat za nyuma space ipo ya kutosha kwa normal Sized people mnakaa comfortable tu, tena bonge kiasi ndo safi. Boot ipo ya kutosha mishangazi kaja inaingia mingi tu na unaweza laza seats incase unataka space Zaidi..
.
Gari ina grade tatu Mitsubishi RVR E, RVR M na RVR G na hizo zote utofauti ni kwenye features zake tu. RVR E ni base grade haina features nyingi, inafatiwa na RVR M na G ndio luxury grade na nitakugusia features zake kwa uchache. Ina rims za inch 17, wenzake E na R ni 16, Ina Multi Information Display(MID ), gear knob yake na steering ni leather..
.
1729078599624.png
1729078609262.png
.
Ina paddle shift for sport Mode, cruise control na armrest siti za nyuma ambayo ni storage box pia na Panorama sunroof. Music pia ni wa tofauti ina Rockford Fosgate Premium Sound System, Wakali wa music wa magari kutoka Marekani hawa. Ukiwa nao no need of woofer Mzee na pia gari ina Super-wide HID headlights, so usiku unateleza tu kama mchana.
.
Twende jikoni sasa ambako ndiko nguvu za kuvimba kwa road zinatoka, gari imekuja na engine option moja 1.8L Petrol. Sema kwenye hizi engine kuna moja iko coded 4B10 na nyingine 4J10 both are good engine but 4J10 ndo latest. Yenyewe ni nyepesi so ina utumiaji mzuri zaidi wa mafuta Na ina mfumo latest na very smooth wa Auto Stop & Go (AS&G) kwa ajili ya kusave mafuta. Hii gari ilienda masoko ya nje pia kama ulaya na marekani so huko kuna engine zingine pia hadi za Diesel. Ila kwa Mama Kizimkazi nakushauri komaa na engine za Japan hizi 4B10 na 4J10 Petrol.
.
1729078756301.png
1729078766715.png
.
Engine zote ziko linked na 6-speed INVECS-III CVT, Hii gearbox inafanya gari kuwa economy na smooth kwa road. Gari ina 2WD, 4WD AUTO na 4WD Lock so kwenye njia korofi unateleza tu as tyre zinapewa traction kutokana na uhitaji [driving condition]. Pia engine zina Mfumo wa MIVEC na hii mifumo ni ya Kisasa inahitaji oil nzuri [genuine oil] ili isisumbue. MIVEC ni kama VVT-i isikuchanganye [Mitsubishi Innovative Valve timing Electronic Control system], Lengo ni ku boost fuel efficiency tu kwa kutoipa engine mafuta pale isipohitajika.
.
Pia engine zake hazina hydraulic lifters so inashauriwa kila baada ya km 50K++ kucheki/adjust valve clearances. Hii kwa lugha nyepesi kuna kidude [valve tappet] na mkono unaokizungusha ndani ya engine inatakiwa iangaliwe iwekwe sawa. Maana as time goes na engine inavyotumika kinakua kinatoka kwenye position yake sitahiki. Hii shida huwa inasabisha gari kuwa na hard start lakini pia silence kuwa ya shida na matumiza mabaya ya mafuta. Na ukiwa unataka kununua/Kuagiza hii gari ukiona ina any sign of oil leakage achana nayo, leakage za kina Kluger ndo unaweza pambana nazo.
.
1729078971673.png
1729078981511.png
.
Tofauti na hapo hizi Engine ni nzuri tu with proper care mtengenezaji anategemea utumie Km 250,000 ndo zianze kuonesha dalili ya kufa..Mafuta gari inatumia vizuri sana tena with 6 speed [simulation] gear box na 1.8L unapata Km 13-15/L, hii ni mtelezo tu..Acceleration yake iko safi inakupa 0-100Km/h in 11.5 sekunde, full tank inakula litre 60 ukitia full unaitafuta Mbarali. Na speaking of stability iko vizuri ina Active Stability Control(ESC) Ya umeme plus iko chini so hata kwenye kona inafanya vizuri. Kwenye safety features inafanya vizuri pia ina Airbag za Magotini Pamoja na pembeni + ina emergency stop signal sytem. Spare zake zinapatika na bei ni Rafiki tu though ziko juu compare na Toyota of the likeS lakini sio bei ya kukukimbiza. Halafu kuna baadhi ya spare wanashare na kaka ake outlander na mpaka idai spare flani utakua usharuka nayo sana maana spare zake ni genuine ukifunga umefunga.
.
1729079227064.png
1729079248510.png
.
Hii machine kuiagiza from Japan ina cost around 21-25M+ kutegemeana na gari husika na sifa zake..Kama unahitaji kuagiza gari njoo tuko na network ya trusted dealers kwa Japan, UK, Singapore, Thailand etc. Dealers wanaotupa gari zenye ubora wa juu kwa bei nzuri kwa ajli yako Pia tuna uzoefu wa kuspot gari nzuri kwenye sites za Japan gari zenye viwango na grades nzuri maana tunashinda mtumbani kila siku. Tutafanya mchakato wako wa kupata gari kuwa rahisi na salama kwa pesa yako na unaojali muda wako. Simply njoo WhatsApp 0714547598 au ofisini Posta Mpya MUA House 4th Floor mkabala na Mkapa tower tutaku assist + kukushauri.
.
1729079401734.png
1729079413587.png
..
Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu, utatupa hitaji lako tutakupa Ushauri pia then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice. Utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo. Natumaini umejifunza kitu kama jibu ni ndio basi usisahau kushare kwa ajili ya wengine. Kama hujatu follow katika kurasa zako za jamii gonga follow sasa @samatimemagari/cardealers ili usipitwe na madini..
.
1729079623088.png
1729079630374.png
1729079642439.png
.
Pia kama una mpango wa kumiliki gari siku za mbeleni njoo whatsapp na jina lako na unakopatikana tutakusave na utakua na direct access ya huduma zetu pamoja na kuona OFA na madini kupitia whatsapp.
.
Asante na tukutakie siku njema
Samatime Magari
0714547598
 
Shida ya wabongo uaminifu zero,unaweza mwamini mtu kupitia maelezo kama haya ukiamini anajua anchokifanya lakini akakushangaza akakupendekezea kitu kibovu huku akikaza kabisa shindi kuwa boss wangu chukua hii ndio yenyewe.imesimama mara kitu kimenyoka na maneno mengi ya kupamba
 
Maelezo mazuri sana mkuu.

Unaizungumziaje ishu ya kelele za nje kusikika sana ndani ya gari hata ufunge vioo?. Naona reviews nyingi YouTube za RVR wanalalamikia hili.
 
Maelezo mazuri sana mkuu.

Unaizungumziaje ishu ya kelele ndani ya gari?. Naona reviews nyingi YouTube za RVR wanalalamikia hili.
Kelele ipi Mkuu weka nyama kidogo hapa as i recall kuna heat shield metal ndo case nyingi watu wamekutana nazo huwa inakua loose inacheza
 
Shida ya wabongo uaminifu zero,unaweza mwamini mtu kupitia maelezo kama haya ukiamini anajua anchokifanya lakini akakushangaza akakupendekezea kitu kibovu huku akikaza kabisa shindi kuwa boss wangu chukua hii ndio yenyewe.imesimama mara kitu kimenyoka na maneno mengi ya kupamba
uko sahihi kwenye kila game kuna wachezaji aina zote ni kuwa makini tu una team up na nani kufanikisha jambo lako
 
Kelele ipi Mkuu weka nyama kidogo hapa as i recall kuna heat shield metal ndo case nyingi watu wamekutana nazo huwa inakua loose inacheza
Nazungumzuia road noise mkuu. Wanasema hata ufunge vioo, kelele za mvumo wa tairi na kelele za nje zinasikika sana kwa ndani.
 
Kwa budget ya 20-25M ni gari gani rafiki kwa matumizi ya kawaida kwa mtu anayeendesha muda mwingi kwenye rough road ?. Ikiwa SUV itapendeza zaidi

Pia iwe imara isiyobugia mafuta.

Samatime Magari
 
Haka kagari nakaelewa sana huu mwaka Mungu anibariki nikapate keupe tu🙏🏾🕯️
 
Back
Top Bottom