YES Tunahitaji Apartments Tanzania Lakini si kila Mkoa

Dah! umeshinda kaka.
 

Unaingiza mambo mengine very controversial. Kwenye research gani huwa mnaangalia asilimia 50? This is a gross oversimplification kwa kweli...

Kitu cha kwanza kinachoweka upungufu mkubwa kwenye hoja zako ni pale unapofanya assumption kwamba kila mtu anatakiwa kuwa mfanyabiashara. Kosa hili huwa linafanywa na watu wengi sana na wakati mwingine hata organisations. Ukiwauliza hawa akina mama tutawasaidia vipi, utasikia jibu lao ni kwamba wapewe mitaji waanzishe biashara!!!

Matokeo yake wale akinamama wanafungua biashara ukija baada ya miezi sita unakuta asilimia 60 tu ndio bado wana biashara, ukija baada ya mwaka unakuta wamebaki asilimia 20, baada ya miaka miwili unakuta wamebaki less than 5 percent. Ukija baada ya miaka mitano unakuta wamebaki less than 2 percent na mpaka mwisho unaweza kukuta waliofanikiwa kutokana na mtaji huo ni watu watatu tu kati ya watu 200.

Kwahiyo hapa kinachoonekana ni kwamba ukitaka kulenga kuojoa hiyo jamii kiuchumi, hatua ya kwanza ni kuidentify hawa watatu wenye ari na uwezo wa kufanya biashara, halafu uwapatie mtaji mkubwa badla ya kuuganwanya kwa watu wasioweza biashara.

The same at family level. Sio kila pesa inatakiwa kufanyiwa active business. Kunakuwa na pesa nyingine inewekwa kama "nest egg". Zipo njia mbalimbali za kutunza pesa. Mojawapo ni kununua appartments.

Ni forces of demand and supply. Waache investors wajenge uone kama hazitanunuliwa na kama watu hawataishi humo. Kama zinanunuliwa na baadae watu wanaishi maana yake zinahitajika, au definition ya kuhitajika ni nini?
 
Appartment ya kwa ajili ya biashara ni ngumu sana kulipa baadhi ya mikoa maana wateja hakuna, mzunguko wa pesa mdogo, wewe ujenge appartment kigoma, songea, tanga, etc utazipangisha kwa bei gani?

Bei ya nyumba/ appartment duniani kote haiangalii uzuri wa hiyo property bali ni location wapi ilipo,,

Nina jamaa yangu wana nyumba masaki inapangishwa usd 2600, sasa sema mkoa gani utapangisha nyumba kwa hiyo bei?

Mzazi ana nyumba tanga ni mpya na nzuri sana but tunapangisha kodi laki 2 tu,, wakati kuna nyumba ubungo ya zamani ilijengwa mwaka 90 inapangishwa kodi laki 5 na nusu kwa mwezi..

Pia aliesema kuhusu yombo na arusha nakupa mfano hai ukitaka nitafute.. Tuna nyumba Vituka ya kawaida tu but inapangishwa laki 4 kwa mwezi... Na watu wanapanga.. Wakati arusha hapo hapo nyumba ya laki 4 au 5 kwa mwezi lazima iwe kali sana.. Sasa hivi hata yombo vituka mitaa ya home chumba na sebule plus jiko tunapangisha 180 na wateja kibao.. Mzazi ana nyumba nyingine mbeya town nzuri kweli kweli lakini hiyo kodi ni majanga inapangishwa laki 2 tu... Kiasi ambapo ingekuwa dar bei ingekuwa mara mbili yake..

Nakupa fact ni biashara ambayo mzazi wangu anafanya,,,

Kama unajenga nyumba / appartment kwa ajili ya biashara kigezo kikubwa cha kwanza ni Location,, demand ya appartment inakuwa determined na location..
 
Angalau nimesoma mjadala wenye tija.
Mleta maada amekuwa na vitu viwili at a time, need appartment, yes...then price? dd & ss? land use and allocation? hata baada ya kupata mawazo ya kobelo, ZeMarcopolo , Prison4664 etc ameshindwa hata kupokewa wazo jipya na hata kusema wengi hatuelewi alimaanisha nini, ingawa amejibu thread nying bado kuna gap.

Mleta maada for now need of housing is unlimited as usaid we all agree, then dd>ss, so we left everything appart, including returns, repayment period, charges etc, for now the saler lead the market!! at the moment we have more sallers, we shall see more changes such as single storey with guarden, sports grounds, surbub buildings etc. for now its just a market forces.
The only thing i am not sure is these buyers how do they afford the price? what is the mortgage system used and what is the main source of capital for the investor? just looking our yet stable financial economy to shrink in case they are invloved in this new business, since I don't know in detail i rest the case for others.
SP
 
Inasemekana kuwa gharama za kujenga apartment moja ni ndogo kulinganisha na gharama za kujenga nyuma moja. Kwa mfano, gharama za kujenga unit moja kwenye apartment ni ndogo kulinganisha na gharama ya nyumba moja iliyo na dimension sawa na hiyo unit. Tofauti na nyumba, kwa kawaida, wamiliki wa units kwenye apartments huwa wana-share gharama za ardhi.

Hata hivyo, bei ya unit moja kwenye apartment haiendani kabisa na gharama zilizotumika kuijenga. Real estators ndiyo wanaonufaika zaidi na hizi apartments. Wanatengeneza faida kubwa kwenye apartments kwa sababu bei ya unit moja kwenye apartment ni sawa na bei ya nyumba moja kwenye sehemu fulani za mji husika.

Kwa hiyo, miradi ya ujenzi wa apartments unaonea kwa kasi Dar na mikoani ni kwa faida ya real estators. Real estators wanafahamu kuwa miaka ijayo apartments hizi zitabomolewa ili kupisha kujengwa kwa nyumba bora za makazi. Lakini kwa sasa wanatumia fursa hii kutengeneza pesa fasta fasta.

Kwa wenzetu waliyajenga miaka hiyo ila sasa wanafanya regeneration kwa kuyabomoa na kujenga nyumba bora za makazi kama ambazo tulikuwa nazo hapa kwetu. Wanadai these apartments are no longer fit for purpose. Lakini kwetu ndiyo kwaaanza apartments are becoming fit for purpose, but perhaps for real estators only.

 
Last edited by a moderator:

Naona umeshinwa kutofautisha investment na business? Unaongelea biashara katika mlengo upi? uchuuzi? Go East, Go West, Go Right, Go left, a house is an investment, japo unapata confusion unapofikiria biashara ya upangishaji as if that is the only return on real estate investment.

[h=2]Mkuu ZeMarcopolo kama una nyumba, Just treat your first home as a real estate investment[/h] In reality, once you buy a property, you become a real estate investor. Buying a home is often considered to be the biggest investment one can make so it is best to treat it as a real investment one which will give you reasonable returns if you do decide to turn it into a rental property or if you sell it further down the road, or mortgaging the same as collateral!
 

Penye RED, ni gap lipi unalosema nimeliacha ili nijibu? Prison4664 inaonesha tunaongelea kitu kile kile lakini katika mlengo tofauti. ZeMarcopolo, tumebaki kwenye ubishi ninapomwambia nyumba ni uwekezaji/investment, na yeye anasema si kila mmiliki nyumba ni mfanyabiashara! Tumeshindwa kuelewana hapo kwamba akinunua kiwanja Segerea akajenga na akaweka mlizi au ndugu na wakaishi bure, bado hataki kukubali kwamba kawekeza japo for the time being hakuna income generation.
 

Yaani wewe mjadala wa jambo kubwa namna hii unauleta down to terminologies!

Acha masihala. Haiwezekani thread nzima wewe peke yako ndio uone watu hawakuelewi lakini uko sahihi!!! Aidha unalazimisha point au unashindwa kujielezea. Chagua mwenyewe where you belong...

Investment kwa jinsi unavyoisema wewe hata kununua viatu pia ni investment. Hata kwenda holiday ni investment. Sasa kama unataka kucheza cheza na maneno, mjadala hauwezi kuwa na conclusion. Tunapojadilia hapa tunafundishana na wanaotusoma pia wanajifunza kwa hiyo lets be more focused kwa manufaa ya wote.

Point ninayoisema ni kwamba si sahihi kusema kwamba kuna mji fulani hauhitaji maghorofa na si sahihi kusema kuwa mikoani ardhi ni plenty. Ufafanuzi wa haya nimeutoa kwenye posts zangu za awali. Nimeendelea kukwambia kwamba sio kila anayenunua au kujenga nyumba ana lengo la kurudisha pesa yake. Mfano mmojawapo ni mimi. Sijawahi hata siku moja kufikiria kurudisha pesa toka kwenye nyumba, lakini ninajua jinsi mipango niliyonayo na hizo nyumba.

Kama una hoja mpya tuendelee kujadili lakini kama unaendelea kulazimisha kuwa wachangiaji hawakuelewi na wewe ndio uko sahihi basi mjadala unapoteza sababu ya kuendelea.
 

Penye BLUE, Nafikiri tuko pamoja!

Penye RED, That is universal, property market value is determined by location, location and location!

Penye GREEN, Masaki apartments zipo hadi za $7,000 nini $2600

Penye RED, kama mzazi wako anafanya mimi kazi ya Real Estate Consultancy ndio inanifanya niende maliwatoni na ni kazi niliyoisomea miaka minne, kwa hiyo naongea kitu ambacho ninakifanya kila siku na ninakielewa. Huko Arusha bei za Nyumba za Njiro zinachuana na Masaki nashanga unasema eti Arusha nyumba ya laki nne au tano ni kali sana. Unaongela Ngaramtoni au Sakina mkuu MKATA KIU?
 

Lakini mkuu hii point yako haitofautishi Dar es Salaam na mikoani. Tunachomkatalia mleta mada ni pale anaposema kwa dar ni OK ila kwa mikoani haihitajiki kwa kisingizio kwamba mikoani kuna ardhi nyingi where as kwenye ardhi ni mashambani ambako thamani ya jengo inakuwa ndogo.
 
Last edited by a moderator:

Sasa unataka nikubaliane tu na hoja yako ili mjadala uendelee? Hutaki kuwa challenged? Mbona kila ambapo mmerise concern nimejaribu kutotoa ufafanuzi, au wewe kwako 1+1=2 not otherwise? Mbona Prison4664 nimemwelewa natukajikuta tunaongelea kitu kimoja? Kama suala ni kukubali unavyotaka wewe ili hoja iendelee, I am sorry Sir!

Naomba ufafanuzi ni kwa vipi kununua viatu ni investment? Unaelewa kwa nini nyumba inaitwa real property na kiatu kinaitwa personal property? Kwa nini usikubali kuelimishwa Zemarcopolo? Mimi akija Daktari au Engineer na hoja yake nitampinga lakini tutakubaliana kwenye facts maana kwa sababu yeye ni mtaalam nitakubali kuelimishwa! Sasa umesema nielezee where do I belong, I belong to Real Estate Economy Profession! And where do you belong Mr. ZeMarcopolo Sir?
 

Le us be honest Zemarcopolo, unaongelea mikoa ipi unaiongelea? Naomba unipe status ya apartments za pale karibu na bunge/Medeli apartments Dodoma? Hizo za Chalinze mnaziongelea unajua zilikaa muda gani mpaka ikabidi kureview price as opposed to projected price? Unasema apartment project inalipa Kigoma na Iringa, kweli? Are you serious?
 

Well, kwangu naona hayahitajiki kote Dar na mikoani kwa sababu tutakuja kuyaboa miaka michache ijayo anyway.

Inawezekana tuna tatizo la ardhi Dar, lakini nafikiri tatizo ni mpangilio mbaya wa jiji.

Kama jiji lilikuwa limepangwa fresh wala tusingehitaji haya makitu.

BTW hivi hizi apartments ziko ndani ya ile master plan ya Dar?
 
Reactions: dig
It comes down to market forces of supply & demand,na sijaelewa kwanini mr expert kaleta hii topic,aim is to discourage watu wasijenge apartments au? na sijui nani alimwambia market ya apartments hakuna mikoani?ila ninachojua hata bila research tatizo la nyumba nzuri za kuishi Tanzania ni kubwa sana ndio maana utakuta watu wana charge ridiculous price kwa nyumba za mbavu ya mbwa,na kitu muhimu kuwa na nyumba sio lazima iwe biashara ya kukuletea monthly rent kujua faida yake,for me its enough just to own it maana nyumba zinapanda thamani kila siku na you can convert into hard cash anytime kuliko kuiweka bank ikaliwa na inflation & banking fees...nawashauri watu wajenge kama wana uwezo.
 
Miji kila siku inakua hata hapo Dodoma/Kigoma etc unaposema after 10 yrs populationa na income za watu zinaweza double or triple,lakini still I don't get it maana ninavyojua tatizo la nyumba za aina zote TZ ni kubwa sana sasa wewe expert naona una discourage watu wasijenge sijui kwa point gani?
 


Tatizo lako unajiona kwamba wewe ni lecturer na wengine ni wanafunzi. Kumbuka kuwa hujui background za wachangiaji wa hii thread. You are a self appointed expert ambaye kitu kikifika asilimia 50 unachukulia kuwa kiko statistically significant.

Hapa umetoa mfano wa maghorofa ya Chalinze lakini statement yako haitoi jibu kwamba iwapo Chalinze zingejengwa nyumba za chini zingeuzika kirahisi. Tatizo la Chalinze ni ghorofa au ni location?
 

Dar master plan ina squares nzuri lakini ukienda unakuta garage na maghorofa. Ni ngumu kujua kama yapo kwa kweli ila nikiambiwa nifanye guess work nitasema hayapo. Oysterbay imeshaanza kugeuzwa high density siku hizi. Sehemu yenye nyumba moja zinajengwa apartments 50. Wakiendelea hivyo Oysterbay kutakuwa kama Kariakoo...
 

Ni ngumu sana mikoa ya Tanzania kukua kufika level ya kupangisha nyumba kama dar es salaam..

Kwa sababu shughuli zote muhimu zinafanyika dar, asilimia 80 ya pato la taifa linatoka dar, gesi inaletwa dar, bandari mpya dar, makampuni ya kigeni as Toyota, sony etc yakija Tanzania head office zinawekwa dar, hushangai hadi Barrick shughuli zake madini lakini head office Dar, kwani ingeshindikana kuwekwa office mikoani, mabasi ya kwenda kasi dar, airport ya kisasa terminal 3 Dar,,

Tukatae, tukubali nchi hii Real state business mikoani ni ngumu kupata wateja kama dar,, mikoani mtu anaelipwa million 3 tu ili aje kupanga appartment kwa kodi nzuri unamtafuta kwa tochi, wakati Dar hiyo ni mishahara ya kawaida sana so watu wana uwezo wa kupanga hizo appartment bila wasi wasi wapo Dar..

Mikoani asilimia kubwa ya wafanyakazi ni halmashauri, NMB, wakufunzi wa vyuo, na subordinates wa kampuni ambazo head office zake zipo Dar.. Wafanyakazi wa mikoani kulipa kodi nzuri kwenye appartment hawawezi wanaona bora wasogee pembeni wajinunulie viwanja kwa million 1 up to 5 then wajenge nyumba zao..

Kwa dar kuna expart kibao ambao appartment ndio option kwao, plus vijana kibao wanaoanza maisha bila kusahau wafanyabiashara kibao ambao wanamudu kodi za appartment bila matatizo,,,

Ni kweli tunahitaji appartment lakini sio kila mkoa.. Unajenga appartment Mpwampwa, Tabora, Tanga, Iringa kwa ajili ya biashara sio wazo sahihi ukifanya cost benefit analysis, ila kama unajijengea tu mradi uwe unamiliki appartment hapo siwezi kukuzuia.. But kama ni for business unafanya uamuzi mbovu
 
Ni wapi nimediscourage watu wasijenge apartments? Umeelewa muktadha wa hoja yangu mkuu?
 

Bado naona hukuiosoma na kuilewa hoja yangu? Kwa hiyo hizo apartments zijengwe zisubiri 10 years? Mimi sijasema ni mwiko kujenga apartments Tunduma na Katavi, no! Hoja yangu zikijengwa leo zitalipa ati kisa zinalipa Dar es Salaam?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…