Barnabas Mashamba
JF-Expert Member
- Jul 4, 2020
- 1,154
- 3,144
- YT shorts kwa sasa ni hadi 3Minutes.
Mwangaluka wanaJF
Ni siku nyingine tena, team ya Yesu Anajibu tunakuletea mazungumzo yaliyofanyika baina ya Ticha Mashamba na Yesu Kristo. Ticha Mashamba alihitaji kujua kwa nini katika kazi zote zilizopo duniani, Yesu Kristo (mshirika katika uumbaji) alichagua kilimo kiwe ndiyo kazi ya kwanza kumpatia binadamu.
kwa wale wasio na bando kufuatilia video ya mazungumzo hayo, hapa kuna mazungumzo kwa ufupi kwa njia ya maandishi.
kwa wenye bando, tembelea katika link ya video hapo chini ili uweze kuyapata mazungumzo hayo kwa urefu.
Mazungumzo kwa ufupi
Ticha Mashamba: Rabi, ni dhahiri kabisa uliumba kila tunachoona hapa duniani, tukiwemo na sisi binadamu.
Rabi: Wewe wasema.
Ticha Mashamba: Baada ya kumuumba mwanadamu wa kwanza ambaye ni Adamu, ulimpatia kazi ya kufanya. Ni kwa nini katika kazi maelfu zilizopo duniani ulimpatia kazi ya ukulima?
Rabi: Nitajibu swali kupitia maswali.
Ticha Mashamba: Karibu sana Rabi kwa maswali, nami nitayajibu kulingana na namna ninavyoyafahamu majibu yake.
Rabi: Wakati natoa kazi ya ukulima kwa Adamu, imeandikwa kulikuwa na watu wangapi bustanini?
Ticha Mashamba: Kwa mujibu wa kitabu cha mwanzo sura ya kwanza hadi ya tatu ndani ya Biblia, Kulikuwa na watu wawili, Adamu na mkewe Hawa.
Rabi: sasa chukulia kwa mfano ningewapa kazi ya kufundisha yaani ualimu, wangewafundisha akina nani wakati bustanini walikuwepo wawili pekee?
Video link
View: https://youtu.be/3eMx4wgXzEs
Take it easy bro.Binafsi nimeogopa kuendelea kusoma, baada ya kuona umeanza kwa kumpa Yesu, sifa za Mungu mmoja mwenye mamlaka yote, kitu ambacho sio sahihi. Hebu tumia akili yako vizuri badala ya kukaririshwa mistari isiyokuwa na uhalisia...
1. Yaani, Yesu aliyezaliwa na Binadamu,
2. Aliyekuwa anakula chakula,
3. Anakwenda choo,
4. Analala usingizi (Yaani Mungu analala kabisa, sasa si anapitwa na mambo mengi?)
5. Anakesha akimuomba MUNGU,
6. Anafunga kumuomba MUNGU amsaidie kutekeleza majukumu aliyopewa na MUNGU
KWA KIUMBE CHENYE SIFA NILIZOTAJA, KUKIITA MUNGU, NI KUDHALILISHA UKUU WA MUNGU KWA KIWANGO CHA JUU KABISA!. Mungu tusamehe kwa kukosa maarifa!
Kuhusu kazi bainadam aliyopewa, nikimaliza kusoma nitachangia tena.....
Ushauri nimeupokea na nitaufanyia kazi kwa haraka.kazi Nzuri,
Keep it up.
[Idea]
- YT bado una subscriber wachache.
- Hakikisha unatengeneza shorts 9:16; Hizi hutembea zaidi na itakusaidia kupat viewers/ subs za kutosha.
- YT shorts kwa sasa ni hadi 3Minutes.
Take it easy bro.
Nimeandika kulingana na ninavyofahamu Mimi.
Kama unaona nimekaririshwa, basi huenda nami naona umekaririshwa maana hakuna hata mmoja Kati yangu na wewe aliyeyaona mambo kwa uhalisia wake kama alivyofundishwa.
Hivyo, kama umefundishwa kuwa Yesu si Mungu, wafanya vyema kufuata na kuamini mafundisho ya Imani yako, nami ninayeamini Yesu ni Mungu, nafanya vyema kufuata mafundisho ya Imani yangu.
Umeeleweka.Mimi sijakaririshwa kwa kuwa nimesoma mwenyewe Biblia kwa takribani 92% bado kido nimalize. NIMEJIRIDHISHA BILA SHAKA KUWA, BAADHI YATAFSIRI TUNAZO PEWA NA WAHUBIRI SIO SAHIHI
KWANI HUSOMA MSITARI MMOJA NA KUISHIA KUTUPA TAFSIRI TOFAUTI KABISA NA ILIYOKUDUDIWA.
Hata kwa akili ya kawaida, Kiumbe chenye sifa tajwa hapo juu hakiwezi kuwa Mungu
Lakini pia ule mstari wa "wewe wa sema" huwa unapewa tafsiri potofu kuwa Yesu alikubali kuwa yeye ni Mungu. Hivi ukiwa mahakamani mtu akikuambia; wewe ni mwizi? ukajibu wewe wasema; haimaanishi kuwa umekubali kuwa wewe ni mwizi? umemaanisha tu kuwa, wewe ndiye uliyesema ila mimi sijasema hilo.
Mwangaluka wanaJF
Ni siku nyingine tena, team ya Yesu Anajibu tunakuletea mazungumzo yaliyofanyika baina ya Ticha Mashamba na Yesu Kristo. Ticha Mashamba alihitaji kujua kwa nini katika kazi zote zilizopo duniani, Yesu Kristo (mshirika katika uumbaji) alichagua kilimo kiwe ndiyo kazi ya kwanza kumpatia binadamu.
kwa wale wasio na bando kufuatilia video ya mazungumzo hayo, hapa kuna mazungumzo kwa ufupi kwa njia ya maandishi.
kwa wenye bando, tembelea katika link ya video hapo chini ili uweze kuyapata mazungumzo hayo kwa urefu.
Mazungumzo kwa ufupi
Ticha Mashamba: Rabi, ni dhahiri kabisa uliumba kila tunachoona hapa duniani, tukiwemo na sisi binadamu.
Rabi: Wewe wasema.
Ticha Mashamba: Baada ya kumuumba mwanadamu wa kwanza ambaye ni Adamu, ulimpatia kazi ya kufanya. Ni kwa nini katika kazi maelfu zilizopo duniani ulimpatia kazi ya ukulima?
Rabi: Nitajibu swali kupitia maswali.
Ticha Mashamba: Karibu sana Rabi kwa maswali, nami nitayajibu kulingana na namna ninavyoyafahamu majibu yake.
Rabi: Wakati natoa kazi ya ukulima kwa Adamu, imeandikwa kulikuwa na watu wangapi bustanini?
Ticha Mashamba: Kwa mujibu wa kitabu cha mwanzo sura ya kwanza hadi ya tatu ndani ya Biblia, Kulikuwa na watu wawili, Adamu na mkewe Hawa.
Rabi: sasa chukulia kwa mfano ningewapa kazi ya kufundisha yaani ualimu, wangewafundisha akina nani wakati bustanini walikuwepo wawili pekee?
"BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza."
Mwanzo 1:28
"Mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani..."
Mwanzo 2:15
"Ailime na kuitunza."
Hiyo ni kazi ya kutambua, kupanga na kuainisha.Mwanzo 2:19-20
Adamu aliwaita majina viumbe wote.
Kwa mantiki ya Ticha Mashamba, mtu angeuliza:"Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi." (Mwanzo 1:28)
"Na maneno haya... uwafundishe watoto wako kwa bidii."
Asante kwa kushiriki mjadala.Hoja hiyo ina tatizo kubwa la kimantiki na kibiblia.
Kwanza, umeanza kwa kudhani kwamba Yesu ndiye aliyekuwa akizungumza na Adamu na ndiye aliyempa kazi ya kulima. Lakini Biblia haisemi hivyo. Biblia inasema ni Mungu (YHWH) aliyemuumba Adamu na kumweka bustanini.
Mwanzo 2:15
Aya haisemi "Yesu akamtwaa Adamu", bali inasema BWANA Mungu.
Pili, swali la "kwa nini hakuwapa ualimu?" halina uzito wa kuthibitisha chochote. Kwa sababu kazi ya kwanza aliyopokea Adamu haikuwa kulima pekee.
Biblia inaonyesha Adamu alipewa majukumu mengi kwa wakati mmoja:
- Kutawala viumbe
Hiyo ni kazi ya utawala.
- Kutunza bustani
Hiyo ni kazi ya uhifadhi na uzalishaji.
- Kuwapa wanyama majina
Hiyo ni kazi ya kutambua, kupanga na kuainisha.
Kwa hiyo si kweli kwamba "kazi ya kwanza ilikuwa kilimo tu."
Tatu, hoja yako kuhusu ualimu inajibiwa na Biblia yenyewe.
Je, walipokuwa wawili tu, Mungu aliwaambia:
Kwa mantiki ya Ticha Mashamba, mtu angeuliza:
"Kwa nini Mungu awaambie waijaze dunia wakati bado walikuwa wawili tu?"
Jibu ni rahisi:
Mungu alikuwa anazungumza kuhusu mpango wa baadaye, si hali ya dakika ile ile.
Vivyo hivyo, kama Mungu angewapa jukumu la kufundisha vizazi vyao, isingekuwa tatizo kwa sababu watoto wao wangekuja baadaye.
Nne, Biblia inaonyesha kwamba jukumu la kufundisha watoto lilitolewa tangu mwanzo wa historia ya mwanadamu.
Kwa mfano:
Kumbukumbu la Torati 6:6-7
Hivyo kufundisha ni sehemu ya mpango wa Mungu; si kwa sababu hakukuwa na wanafunzi wakati Adamu alipoumbwa.
Mwisho, kama lengo la simulizi hili ni kuthibitisha kuwa Yesu ndiye aliyempa Adamu kazi kwa sababu ni "mshirika wa uumbaji", basi hilo linahitaji uthibitisho wa moja kwa moja kutoka Biblia. Hakuna aya inayosema:
"Yesu alimwambia Adamu: ailime bustani."
Biblia inasema ni BWANA Mungu aliyefanya hivyo.
Kwa mtazamo wa Uislamu, Qur'an pia inafundisha kuwa Adamu aliumbwa na Allah peke yake, na Allah ndiye aliyemfundisha na kumuamrisha (Qur'an 2:30-33; 2:35), si Yesu.
Kwa hiyo, hoja hii haithibitishi uungu wa Yesu. Inajenga hitimisho juu ya dhana ambayo Biblia yenyewe haijasema.
Asante kwa kushiriki mjadala.
Kwenye Kiswahili Kuna kakipengele kanaitwa "Fasihi". Kama elimu yako ulisomea hapa Tanzania itakuwa unakafahamu kakipengele hako. Kama ndivyo, tafakari.