Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
sio kwamba haelewi maandiko,bali unamtaka ayaelewe unavyoelewa wewe na asihojihoji zaidi,
pia umetoa maelezo yako na unahisi maelezo yako ndio final,
sasa anakwambia lete ushahidi,hakubaliani na maelezo yako
Hakuna mahali nimemtaka akubaliane na mimi, mimi namueleza msingi wa imani ya kikristo ulipo, labda yeye aniambie anataka jibu gani!!.

Hili ni tatizo la kuuliza swali ukiwa na majibu yako kichwani.anataka ushahidi wa maandiko, akiletewa anasema bible haijashushwa hivyo haamini.
 
sio wakristo wote wanaamini yesu ni mungu?,labda wawe wameanza kuamini mwezi uliopita
 
Acha utoto wewe kama kweli yeye mungu mbona alivyokuwa msalabani akasema mungu wangu mungu wangu mbona umeniacha kama yeye ni mungu na huyu aliye kuwa anamlalamikia ni nani?nikuongeze kitu kingine mungu gani anakaa tumboni miez 9,anakula anakunywa a naenda haja dah .umeharibiwa akili na vitabu walivyotunga wajanja.lete hoja nikuelewa Acha kufikiri kwa ma kalio ww aafu unakuja hapa kutokwa povu we unaona umejiiibu Acha uk******laza
 

Sikushangai hizi ni akili sampuli ya mohamed kabisa hizi.

Huu uzi uko posti ya ngapi, tuko tunafafanua haya maswali yako ya watoto wa sundayschool husomi uelewe, badala yake unakuja kuquote baba zako kihunihuni tu.

Haya rudi kaanze upya.
 
sio wakristo wote wanaamini yesu ni mungu?,labda wawe wameanza kuamini mwezi uliopita
Sasa kama ukristo kwake ni kuitwa john na kwenda kanisani!!!!, huyu hata ukikaa naye atakueleza nini cha maana, zaidi ya kukusifu kwa kuruhusiwa kuoa wake wengi?!!????
 
Nawaza tu
1. Kwa kuwa Yesu ni Mungu na Mungu huyo alizaliwa na bikira Maria basi nathubutu kusema bikira Maria ni mkubwa kuliko Yesu(Mungu) maana mtoto kwa mama atabaki kuwa mtoto tu. Hivyo utukufu wa juu kabisa ni wake Maria maana ndo aliyemzaa Mungu wenu.

2. Kwa mujibu wa maandiko yenu, Yesu alikufa na siku ya tatu akafufuka. Hiyo ina maana kuwa dunia ilikaa siku 3 bila Mungu. Je nani aliiongoza dunia kwa muda huo wa siku 3?

4. Ninavyofaham uwezo wa Mungu hauna limit, ana uwezo wa kujua ya jana ,leo na kesho, hivyo Yesu(kama kweli ni Mungu) kabla ya ujio wake duniani alishaona kitakachomtokea. Kwani alikubali kuja kudhalilika? Kwanini aliionesha dunia kuna watu wana uwezo zaidi yake (waliomtesa msalabani) ilhali ye ni Mungu muweza wa yote.

3. Kama kweli yeye Yesu ni Mungu kwanini alikuja dunian? Kwanini alishindwa kuuumba kiumbe chenye uwezo wa kufanya hiyo kazi iliyomleta yeye duniani? Haoni kuwa kitendo cha yeye kuja duniani na kuteswa kama viumbe wengine dhaifu kimechangia kupunguza imaani kwa baadhi ya watu (mfano Mimi siamini kabisa Mungu muweza wa yote anaweza kuteswa na kiumbe alichokiumba mwenyewe)
Maswali ni mengi lkn acha niishie hapa [emoji124]
 
Hivi huko nako huwa mnafundishwa kampeni?????

Sasa kama hii ni kopy original unayo tuisome hapa????
Kwani hujui kama kuna version tofauti za bible? na zimeongezwa na kupunguzwa maneno
 
Ulitaka auite ufalme wake dogo au bro????
Haya bwana na mungu wenu anayeuchapa usingizi hadi wanafunzi wanataka wafe baharini sasa sijui wakati mungu amelala nani alikuwa anaongoza ulimwengu, halafu Waisrael Noma sana yani hawamtaki mungu wao wanamtaka barabaaaa.
 
Haya bwana na mungu wenu anayeuchapa usingizi hadi wanafunzi wanataka wafe baharini sasa sijui wakati mungu amelala nani alikuwa anaongoza ulimwengu, halafu Waisrael Noma sana yani hawamtaki mungu wao wanamtaka barabaaaa.
Wewe mwenyewe unamkana sjui unamtaka nani????
 

Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahim na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo uwape neema yako wale wasiokufahamu, wakufahamu, wakukiri na wakutumikie ili waokoke. Wale wenye kiburi uwalegeze mioyo yao ili warudi kwako na wasipotee na waliolegea katika IMANI uwape nguvu ya kukutumikia kwa uaminifu. Amen.
 
Sikushangai hizi ni akili sampuli ya mohamed kabisa hizi.

Huu uzi uko posti ya ngapi, tuko tunafafanua haya maswali yako ya watoto wa sundayschool husomi uelewe, badala yake unakuja kuquote baba zako kihunihuni tu.

Haya rudi kaanze upya.
anyway ngoja nikuache kama ulivyo coz akili chache haiwezi ongoza akili nyingi ok my in law gooday
 
Kabla hatujamsaidia huyu mwenye mada mwenye mashaka. Tumuulize Mungu ninani kwanza.
 
Alivyokua duniani Yesu alijivua uungu. Ndo mana akawa anamtegemea Mungu baba!
Angekua Mungu akati yuko duniani hasingezaliwa, hasingesikia njaa, hasingeweza jaribiwa na hasingekufa. Yesu alichukua ubinadamu ili aishi duniani.
Unaonesha jinsi gani ulivyokosa akili ya kutafakari. Yaani umesema kwamba yesu alivyokuwa duniani alikuwa anamtegemea mungu baba. Jibu lako tu linaoonesha kuwa kumbe kuna mwingine zaidi ya yesu alikuwa ndio kila kitu na ndio Mungu huyo. Kwani una miungu mingapi wewe? Maana kuja kwa yesu duniani nilijua utasema kuwa alijitegemea mwenyewe kwavile alijivua uungu. Kumbe ana mtegemea baba. Sasa hapo mkuu ni baba na sio yesu. Je yesu ni nani? Haaa ni mtumishi tu wa Mungu.

Matendo 3:13

Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe

Matendo 3:26

Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake
 


Asili ya imani ya mungu-mtu na desturi zake


Kulingana na mafundisho ya Biblia tukufu, asili ya imani ya mungu-mtu imetokana na watu wa mataifa, yaani wapagani ambao wengi wao ndio ambao hawakubahatika kufikiwa na ujumbe wa Mungu-Yehovah kupitia msururu wa Manabii wake ambao kwa idadi kubwa aliwatuma kwa wana wa Israeli.

Kwa hali hiyo, ni wazi kuwa watu hawa (wa mataifa au wapagani) walikuwa mbali kabisa na Mungu-Yehovah kwa kutomjua na kwa hiyo wakaangukia katika imani potofu ya kuamini miungu bandia yenye desturi za kujigeuza kuwa mfano wa wanadamu.

Uthibitisho wa hayo tunaupata katika maandiko ya Biblia tukufu yafuatayo:


"Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamake, ambaye hajaenda kabisa. Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena, ambaye akamkazia macho na kuona kuwa ana imani ya kuponywa, akasema kwa sauti kuu, simama kwa miguu yako sawa sawa. Akasimama upesi akaenda. Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu. Wakamwita Barnaba, Zeu na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji. Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano". (Matendo ya Mitume 14:8-13)


Tunachoelezwa na maandiko hayo ya Biblia Tukufu hapo juu ni kwamba, Bwana Paulo na mwenzie Barnaba walipofika Listra (huko kwa watu wa mataifa au wapagani) waliwakuta wenyeji wa huko tayari walikuwa na dini yao yenye miungu iliyokuwa na tabia ya kujigeuza kuwa wanadamu.

Miungu hiyo ambayo tayari ilikuwa na majina yao kama hayo ya Zeu na Herme, walikuta pia tayari imewekewa taratibu za dini, ikiwemo hiyo ya kuwa na mahekalu.

Aidha, waliikuta dini yao hiyo tayari imewekewa pia utaratibu wake wa ibada wanazoifanyia miungu yao hiyo; kama hiyo ya kuitolea miungu hiyo dhabihu kwa kuichinjia wanyama na kadhalika.

Maelezo hayo ya Biblia vile vile yanaonyesha pia kuwa kwa kuathiriwa na imani yao hiyo ya miungu-watu, watu hao (wa mataifa au wapagani) walipokuwa wakimwona mtu afanyaye maajabu, basi humwita mtu huyo kuwa ni mungu kwa majina ya miungu yao hiyo (akina Zeu na Herme) kama walivyowaita hapo kina Paulo na mwenzie Barnaba kwa kuona jinsi walivyomfanyia maajabu kiwete.

Kwa kuwa waliamini kuwa miungu yao ndio ifanyayo hivyo.

Kwa ujumla basi, hiyo ndiyo hali halisi aliyoikuta Bwana Paulo na mwenzie Barnaba kwa watu wa mataifa yaani wapagani.

Kwa shuhuda hiyo ya Biblia, tunaona wazi kuwa asili ya imani ya mungu-mtu mwenye desturi ya kujigeuza mwanadamu inatokana na watu wa mataifa, yaani wapagani.
 
mkorinto:

Sifa kuu za miungu-watu wa wapagani


Kwa mujibu wa Bwana Paulo (kama tutakavyokuja kuona hapo baadae) miungu-watu hii (kama hiyo ya akina Zeu na Herme) ilikuwa na sifa kuu zifuatazo:

Kuzaliwa na mwanamke

Kuwa na sifa zote za mwanadamu (kama vile kula, kunywa, kulala, kwenda choo, kuchoka na kadhalika).

Kujibadilisha-badilisha (wakati fulani inakuwa miungu na wakati mwingine inakuwa wanadamu).
Kufa na Kufufuka.

Kwa wanaotaka kupata taarifa zaidi kuhusu sifa hizi za miungu-watu kama zilivyoelezwa na Bwana Paulo, wasome taarifa zaidi kutoka "Encyclopaedia Brittanica" chini ya maneno Zeus na Hermes (Jupiter na Mercury).
 
mkorinto:



Dini ya Kikristo na imani ya mungu-mtu


Awali kabisa tumeona maandiko ya Biblia tukufu yakielezea jinsi Bwana Paulo na mwenzie Barnaba walivyokwenda kwa watu wa mataifa, yaani wapagani na kuwakuta watu hao tayari wanayo dini yao yenye miungu iliyokuwa na tabia ya kujigeuza kuwa wanadamu.

Sambamba na dini hiyo (ya wapagani), Biblia pia inafundisha kuwa miaka miwili baada ya Nabii Isa au Yesu (a.s.) kuondoka, Bwana Paulo naye alileta duniani dini mpya ya mungu-mtu (kama tutakavyokuja kuona hapo baadae) mwenye desturi naye ya kujigeuza kuwa mfano wa wanadamu.

Dini hiyo aliyoianzisha Paulo aliita "Ukristo". (Tazama Biblia ya Wakatoliki, Imprimatur Mihayo, 1967 Tabora Uk. 1025).

Pamoja na shuhuda hiyo, pia kulingana na mafundisho yake (kama tutakavyokuja kuona kwa kirefu zaidi hapo baadae), ukiondoa majina yao, mungu huyo aliyekuja kumhubiri Paulo, kimsingi hakutofautiana kabisa na miungu hiyo ya wapagani.

Na kwa ujumla basi, ibada nyingi kama si zote za dini ya mungu wake huyo (ya Ukristo) kimsingi zinalingana sawa na zile ibada za watu wa mataifa (wapagani).
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…