Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,443
- 3,480
Nahitaji ushauri kuhusu jinsi ya kuishi na mpenzi aliye mbali (distance love). Kiukweli, naona kama tunadanganyana tu. Kila mara ni "nakupenda, nakupenda," lakini mimi ninahisi hali ni tofauti, kwamba huko aliko, labda anahusiana na mtu mwingine.
Mwanamke huyu si wa kumuamini kabisa, ila mimi nimenyooka sana. Suala la kupiga mademu halipo kabisa kwangu kwa sasa.
Yeye yupo Mwanza, na mimi nipo Tanga. Sasa, je, haya ni mapenzi au kudanganyana tu? Ninajikuta nikihangaika kuelewa maana ya uhusiano wetu. Ikumbukwe kwamba mwanamke mwenyewe ndiye aliyenitafuta na kuniambia kuwa ananipenda.
Kwa kuona heshima hiyo, sikuona sababu ya kumkataa, lakini sasa najikuta na maswali mengi kuhusu uaminifu wake na mustakabali wa uhusiano wetu.
Naomba ushauri. 🙏