Yondo sister wangu nimekukumbuka sana

Yondo sister wangu nimekukumbuka sana

benteke

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
1,305
Reaction score
1,068
Ah... nimekukumbuka kweli Yondo mpaka asubuhi wakati niko njiani nikaanza kucheka mwenyewe.... walikua wananiita Kanda bongo man na wewe walikuita Yondo sister... pale kijiji ilikua kunzia ubatizo, ubarikio, kipaimara na hata ndoa ilikua hatuachwi... walifikiria uhusiano wetu ulikua tu jukwaani kumbe hata nyuma ya jukwaa tulikua wapenzi.

Nilikua nikija tu kwenu mama akiniona tu kabla sijasema kitu basi alikua akikuita.... Yondooo... njoo huku mwenzio kaja kukuchukua muende mazoezi... mazoezi yenyewe hayakuishia kudansi tu. Nakumbuka sana ile staili ya mimi nakua kama naangalia juu ningeng'ata kidole kimoja na meno na huku kidole cha mkono mwingine kikiwa kinazunguka juu kama feni... wakati huo wewe ulikua unapita chini ya miiguu yangu... kwa kweli nimekukumbuka yondo.

Nasikia uko huku mjini na mambo yako ni mazuri sana.
 
Tatizo la kupotezana na Yondo wako ilikuwa nini?
 
Tatizo la kupotezana na Yondo wako ilikuwa nini?

Si unajua tena mambo ya shule,tulitoka kijijini kila mtu alienda kivyake. Hiyo ilikua ni baada ya kumaliza secondary.
 
Ukimpata yondo wako mnialike japo show moja.

serious popote ntakapokutana naye hata iwe posta lazima nimuombe tushtue kidogo.....ilikua raha sana kipindi hicho. sio hichi kipindi cha facebook
 
kama nakuona kanda bongo man ha ha ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom