Yondo Sister yupo hai? Naombeni historia yake

Mkuu Dally Kimoko anatisha ,sikiliza Bilalala-Pepe Kalle, Kin Night au Nairobi Night.

African Ball, wimbo wa Loketho Group chini ya Aurlus Mabele, gitaa alilopiga Dally Kimoko alibadilisha mipigo mara33, mipigo na beats tofauti zote 33 zikiwa kali na hazifanani. Kiukweli Dally Kimoko anasifika kwa kupiga mpini(gitaa). Tumia You tube au kama una CD-VCD-DVD cheza huo wimbo -African Ball- Loketho Group& Aurlus Mabele halafu sikiliza kwa makini mipini ni hatari.
 
Mkuu ni African Ball au Extra Ball ambapo guitar limepigwa na Diblo hata amebadilisha guitar mara nyingi. Pia nakumbuka hata Isabelle pia amepiga Diblo. Kusema ukweli hizi Bongo fleva zimakuja kuondoa raha ya Jiji, upuuzi mtupu. Hebu jiridhishe, hii miaka late 80s na mapema 90 nakumbuka vema. Dar ilikuwa raha kipindi hicho siyo karaha kama sasa. Cheki data zako vizuri mkuu. Nadhani Kimoko mamefanya balaa kwenye Embargo, Loketo &Aurlus Mabele au?
 

extra ball solo imepigwa na mchawi wa nyuzi Diblo Dibala Machacha .huu wimbo hata dally kimoko mwenyewe aliyoosha mikono kwa diblo
 
Hahaha!
Kweli tupu jamani.
Mwanae tunakaa nae hapa Manyanya mtaa wa Mateja, Wibu nyumba no. 216.

Kumbe unaishi kwa Manyanya...sikuwezi, ile mitaa nikipita usiku mnene nawaza sana!!
 

Gatho yupo USA, mambo ya dini kwa sasa.
 
historia ya yondo sister mkuu

Aah kaka, najua kiduchu tu kaka. Yondo sister kama nilivyosema, yupo hai. Kimuziki alikuwa na kundi lake na wanenguaji wake. Wapiga gitaa aliowatumia sana kwa kutegemea album walikuwa ni Dally Kimoko na Shimita. Album kubwa za Yondo Sister ni Mbuta Mutu, Bazo na Madi. Muda mwingi alikuwa na kundi la Soukouss Stars hasa ile Album ya Monerita ambayo ilizinduuliwa kule USA miaka ile ya 1995-1996, ambayo ilikuwa na vibao vikali kabisa kama Monerita, Sophia, Rose, Abagimo n.k. Kwa maelezo yake yeye mwenyewe anasema wale magwiji waliounda ile Soukouss Stars wako kule Ufaransa na wako fit kimuziki japo umri umeenda. Kwa kifupi kabisa ndo hayo kaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…