You are not stuck in traffic, you are the traffic

Wanaosema maendeleo ni kuwa na magari kibao kila mtu yake, wanakosea sana. Nadhani sasa tunaona first hand umuhimu wa kila mtu kuwa na space yake ya kutosha kuleeee mahali instead of kujirundika wooote mijini & majijini na kuishia kuwa chambo na wahanga wa wanasiasa hewa, wachuuzi & wafanyabiashara walafi, majambazi katili, vibaka wenye njaa na hasira ya kukosea gia ya mpando wa maisha, kelele zisizokoma za magari, boda zenye eksozi pana, na hata madai ya malipo kwa upande wa wenye nyumba & pango, vurugu, fujo na ghasia nenda rudi, uchafuzi wa mazingira uliokithiri, matrafiki officers wasiokuwa na weledi wala maadili, Tìiaraei wapigaji pamoja na unyemelezi mkubwa wa magonjwa na maambukizi hatari kama vile korona au ^U-key-mwi^ plus mengine mengi kama hili la kutafuta ajira iliyojaa tumbuatumbua holela na isiyo na mantiki aifanyayo Bi Mkubwa. Au nasema uongo ndugu zangu!???
 
Ndio maana kuna nchi vimeenda mbali zaid had wameamua kutoa usafiri wa umma kuwa bure ili kumshawishi watu kupunguza matumiz ya gari zao pasipokuwa na ulazima
 
Ndio maana kuna nchi vimeenda mbali zaid had wameamua kutoa usafiri wa umma kuwa bure ili kumshawishi watu kupunguza matumiz ya gari zao pasipokuwa na ulazima
Mfano ni Sweeden
 
Si kweli, Sweden public transport unalipia, either unatumia bus card yako ambayo umeilipia kabisa na hela ikiisha lazima uweke tena au utalipa kwa card yako ya bank!
Ndio nlichanganya.usafiri wa Bure upo Luxemburg.
 
Tuanze kampeni ya acha gari nyumbani, tumia baiskeli.
Changamoto Ni kwa wale wanaotoka Kibaha wanafanya kazi Oysterbay
 
Tuanze kampeni ya acha gari nyumbani, tumia baiskeli.
Changamoto Ni kwa wale wanaotoka Kibaha wanafanya kazi Oysterbay
Mimi siku hizi nshazoea mara nyingi gari naacha nyumbani, huwa nikifikiria tu habar ya parking naona isiwe shida
 
Imeeleweka sana... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…