Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kwema Wakuu,
Utaratibu mpya wa TFF unasema kua endapo mshindi wa Azam Sport Federation Cup maarufu kama FA Cup atakua ndio huyohuyo mshindi wa Vodacom Premier League (Ligi Kuu) basi atakaekua nafasi ya pili VPL ndio ataenda Shirikisho.
Ndio kusema kua kama utaratibu huu ungeanza kutumika mwaka mmoja nyuma basi Yanga ndio angekua anatuwakilisha kimataifa badala ya Namungo. Maana Simba alikua wa Kwanza VPL na FA, na Yanga alikua wa Pili VPL huku Namungo akiwa wa Pili FA.
Sasa kwa kasi ya sasa ya Simba ni wazi kua atabeba vikombe vyote hivi viwili kama mwaka Jana, hakuna wa kuizuia iwe mwaka huu na hata mwakani. Labda Simba wenyewe waamue tu wasibebe kombe mojawapo hasa FA kama ntakavyoleza hapa chini.
Najaribu kupiga hesabu hapa naona zinaibeba Yanga kwenye kombe la Shirikisho. Sababu endapo ikafanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye VPL.
Njia pekee ya Yanga kutocheza Kombe la Shirikisho (kucheza Klabu Bingwa hio hawezi) ni endapo atatolewa kombe la FA kisha Simba afungwe (ajifungishe) fainali ya FA. Hapo ni atakaekua bingwa wa FA ndo atakaecheza Shirikisho.
Je Simba atakubali kuliachia hilo kombe ambapo akilishinda itambeba Yanga kama mshindi wa pili VPL??
Kwa hiyo watani zangu hawa wanaweza nao kuanza kupanda ndege kwa nafasi "ya kupewa" hata kama wasipokua washindi wa kombe lolote bila hata ya kusubiri zile nafasi 4 za upendeleo.