Young Africans SC yakodishwa rasmi kwa Yusuf Manji

Jamani, Manji kajiandaa lakini? Maana hii ni timu iliyoleta uhuru nchi hii. Kwamba kina Kifukwe na Wadhamini wenzake wamebeba jukumu zito juu ya hii klabu yetu. HATUTEGEMEI WACHEMSHE HALAFU HUKO MBELENI SIJUI OOOH ILIKUWA HIVI IKAWA VILE, OVAA!
 
Uwanja .m100 kila mwaka...miaka 10=1bil labda cha mazoezi tu
 
Inakulaje kwa Yanga baba?!
 
Kwa hiyo mkopeshwaji hatahusika katika ujenzi wala ukarabati wa nyumba na kiwanja cha pale twiga?
 
Kwa hiyo mkopeshwaji hatahusika katika ujenzi wala ukarabati wa nyumba na kiwanja cha pale twiga?
Ndio majibu na kama akijenga basi kiwanja kitakuwa Mali yake na si Mali ya yanga na mkataba ukiisha jamaa anachukua vyake na yanga wanachukua vyakevyake

Embu jiulize mkuu hilo deni limetoka wapi?? Ni zile hela alizojidai anatusaidia kumbe mwenzetu alikuwa anahesabu kma deni
 
kuna mahali ametajwa manji ndio anadai?
 
Mkuu wamenifurahisha hapo eti Yanga italipwa 25% ambayo watauitumia kujenga uwanja,sasa mbona mkodishwaji anachukua hela nyingi bila kuwa na majukumu ya maana sana?
 
Ni jambo la maana kuifanya timu iweze kujiendesha yenyewe na sio misaada kama ilivyokuwa zamani,lakini nahisi kuna vitu haviko sawa.

1. Deni linalodaiwa limeshawahi kuhakikiwa ..........???
2.Ukomo wa deni ni lini,au hata kama miaka yake 10 hajaweza kulipa basi linahamia kwa wamiliki au wakodishwaji wengine ..........??
3. Nani msimamizi wa huu mkataba kwa pande zote 2 .......??
4.Je, huo mkataba unarithiwa.........Siombei mabaya lakini kwa mungu linawezekana kuwa Manji akafa,inamaana, atarithi mtoto wake au mke wake maana mkataba upo kimya kuhusu hilo jambo.
 
Ni ajabu kwa mkataba kama huu kusainiwa katika karne hii ya 21
 
  1. Mkodishwaji atailipia YANGA deni la Shilingi bilioni kumi na moja na milioni mia sita na sabini na sita tu (Tshs. 11,676 billioni) inayodaiwa kama Mmiliki na Mkopeshaji mmoja.
  2. Mkodishwaji atailipa YANGA Tshs 100 millioni kwa mwaka ambayo YANGA itawekeza kiwango kisichopungua (90%) ili kuimarisha mtandao wa Matawi yake.
  3. Mkodishwaji atailipa YANGA katika mwaka wa fedha wowote ule kukiwa kuna faida ya fedha taslim ya asilimia 25% fedha ambayo YANGA itaitumia kujenga uwanja wake wa mpira.
  4. Mkodishwaji atalipa hasara za uendeshadji zilizoko katika Mkataba kutoka kwenye mfuko wake bila ya kuweka madai kwa YANGA.
  5. Mkodishwaji ataanza kuwekeza kwa vitega uchumi kuanzia siku (90) ya Mkataba katika mafunzo na vifaa, ambavyo kutakuwepo kiwanja cha mafunzo ya mpira katika sehemu atakayo ona inafaa kwake yeye Mkodishwaji.
  6. Mkodishwaji atahakikisha kuwa majukumu yote ya kifedha ya Timu ya Soka ya YANGA ikijumlishwa ada ya usajili zinazotakiwa kuanzia Tarehe ya Ufanisi na majukumu mengine ya siku zijazo yanalipwa kulingana na mahitaji ya YANGA mapema kutoka kwenye mfuko wa Mkodishwaji.






 
nikisoma comments za wengi hapo nagundua kuna tatizo kubwa sana katika kufikiria kwa watanzania. na ni kweli asilimia 90 ya mashabiki wa mpira hawana elimu zaidi zaidi ya shule ya msingi na form four. ni aibu mtu mzima anashangilia mkataba wa hovyo namna hii hapa duniani. ni aibu sana. yaani kuna mtu kabisa ni baba wa familia anampongeza na kushukuru manji kwa huu mkataba?nani kawaroga watanzania? huyu manji hizi akili alizitoa wapi? asilimia 95 wanaona kama hapa yanga imewin. jamani....mbona mnatuaibisha hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…