Hata mimi huwa sielewi! Timu imecheza vizuri, washambuliaji wameshindwa kutumbukiza mpira nyavuni, hapa kocha utamlaumu kwa lipi? Au kwa kuwa hajawachezesha wachezaji (Tegete, Kisambale, Gumbo, n.k.), ambao tunadhani wangeisaidia timu kupata ushindi?
Mimi naamini kwenye mpira lolote laweza kutokea! Mechi ya marudiano Yanga wakicheza kama juzi na kuongeza bidii, YOTE YANAWEZEKANA! Cha muhimu kwa kocha ni kuwaanda kina tegete pia, ili kuwachanganya waarabu ambao tayari wameshawasoma kina Asamoah!