Young D na Tunda Wamwagana rasmi

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,479
Reaction score
1,348


MUUZA sura macha-chari Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kumwagana na mwandani wake wa muda mrefu, ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ na kusema ameamua kujiweka kando kwenye maswala ya mapenzi.

Akipiga stori na ubuyu baada ya kumbananisha kuhusiana na tetesi za uhusiano wake kuvunjika kutokana Young D kubaini anatoka na mwanamuziki mwenziye (jina kapuni) ndipo akaeleza kuwa, ishu hiyo haina ukweli ila ameachana na mwandani wake huyo kwa sababu ambazo hawezi kuzianika kwa sasa.

“Hayo ya kutoka na huyo msanii si kweli na kuhusu Young D nimeshaachana, sifikirii kuwa na msanii yeyote na sihitaji mpenzi kwa sasa,” alisema.
 
Kimpango, kwani walivyoombana tamuu tulikuwepo?
 
Kuna jingine au ni hilo tu?
 
Hawa watoto wanasoma saa ngapi mbona sura za kuwa form 6 au chuo mwaka wa kwanza hizi?

Siku si nyingi unasikia wanagombea ubunge na wanashinda halafu mtegemee nchi iendelee
 
Hawa kina YOUNG wananchanganya kidogo, ni D ama KILLER ambae tumepata hasara wanaume?
 
Kwa hiyo walikuwa wanafanya mchezo mbaya au?
Wazazi wao wanazungumzaje kuhusu hili?
 
😶😶😑😑
Nimefika Pale Njiani Nakuta Lijamaa Limemkumbatia Binti
Angekuwa Binti Yangu Nikitelemka Kwenye Gari Nikazaba Wote Makofi. Lijamaa Halijatoa Mahari
Ndugu Zangu Huu Ndiyo Ukweli Wenyewe
Akiwa Chuo Cha MUST Mbeya
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…