Young Killer matunzo yamekubali, muziki unataka kukukataa

Young Killer matunzo yamekubali, muziki unataka kukukataa

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
Kiwanda cha muziki, lazima tukubali, mara ya mwisho kimetengeneza msanii ambaye kinaweza kikajitutumua na kujisifia kwaajili yake ni kilipomtambulisha "Erick Msodoki" kwa watanzania! Wengi tunamfahamu kama Young Killer, Mimi namuitaga King of Puns - Dogo anacheza na maneno sana kiasi kwamba unaweza kujiuliza alikuwa anawaza nini hadi kuandika hicho alichokiandika.

Nilianza kuwa shabiki yake zamani kidogo kwa hivyo nina facts zake ndogo ndogo ninazozifahamu. Moja na iliyonipa Tittle ya huu uzi ni kuwa: Zamani kidogo kipindi ambacho alikuwa anaanza muziki alijipa a.k.a kibao ila kubwa iliyovuma ni ile ya "handsome boy asiyekuwa na matunzo". Tukaenda na hilo jina mpaka likazoeleka hadi kwenye medias kubwa kwa kiasi cha kulifanya likawa la kwake kabisa. Akatutambulishia "Matunzo zero unit" kuonesha ni kiasi gani alivyo hana matunzo. Basi kwenye hii phase huyu ndugu yangu alitupa ladha, mistari na muziki ambao tulikuwa tunautaka. Naongelea hits kama "13", " Umebadilika", "My Power", " Dear Gambe", na zingine nyingi nyingi sana!

Kusema kweli tulifaidi ladha ya hip hop. Na ni ukweli usiopingika Young Killer ni moja kati ya wasanii ambao wamefanya muziki wa hip hop uwe na mashabiki - Nawajua washkaji baadhi na mademu kadhaa ambao wao hip hop haikumaanisha chochote hadi walipomsikiliza Young Killer na mitazamo yao juu ya huu muziki ukabadilika!

Sasa hapa kati sijui ikawaje?? Ni ghafla tu the kid switched. Kuna intavyuu moja pale Wasafi FM, kama kumbu kumbu zangu hazinidanganyi, jamaa alisema matunzo yamekubali kwa hivyo akatangaza rasmi yeye sio "Handsome boy aliekosa matunzo" kuanzia pale na kuendelea and that was that. Ilikuwa intavyuu nzuri, lazima nikubali na hoja yangu kubwa sio yeye kubadilisha jina ila najaribu kutumia lugha ya picha kuelekeza hili suala ili lieleweke.

By the time anatangaza uamuzi ule alikuwa ameachia Jitafute. Kwa hivyo tukasubiria wimbo ambao utabeba utambulisho wa handsome boy mwenye matunzo hatimae jana ikafika, nikiwa YouTube nikaona hio inayoitwa "Leo". Binafsi mimi sio prodyuza ila ile ngoma nitaiweka kwenye kundi la trap - sio hip hop. Na sio yule Young Killer tunaemtaka. Period.

Bro, sisemi ameshuka ila namkumbusha tu hizo michezo za trap awaachie hao watoto watoto kina OMG, Country Boy na Chin Bees. He is better than that!
 
Young killer ni fundi na ni mtu mbunifu anayebadilikabadilika so simuoni akishuka kimziki na soko linavyotaka usizoeleke na hiyo trap mbona ni wimbo mzuri tu ndo maana aslay sasa ameisha kimziki cos hajui kubadilika.
 
Young killer ni fundi na ni mtu mbunifu anayebadilikabadilika so simuoni akishuka kimziki na soko linavyotaka usizoeleke na hiyo trap mbona ni wimbo mzuri tu ndo maana aslay sasa ameisha kimziki cos hajui kubadilika.
Hakuna pahala nimetaja neno kuwa Young Killer kashuka. Kasome tena uelewe, boss.
 
Kweli mkuu namimi nishabiki wake saaana ila sikuizi anacho imba simuelewi. yaani anaenda kuimba na gigy money[emoji16][emoji1787][emoji23]nyimbo haieleweki nyimbo ya mwisho ya young killer ni sinaga swagg 3
Tatizo sio kaimba na nani? Tatizo ni kaimba nini?
 
Young killer ni rapper flan nomaa kiroho safi ila kuwaita OMG , country boy na chin bees ni watoto kwa msodoki umezingua
 
Sina swaga 3 ndo ngoma ya mwisho imebidi akaze huko huko ndo tunamuelewa
 
Umezingua vile vile kumlinganisha young killer wa HIP HOP na hao wafanya singeli ya kimarekani
Kiufupi umem disrespect
Cja walinganisha ila hata wao kweny angle yao wana ukubwa wao vile vile na sio hicho cheo cha utoto mnacho jaribu kuwapa
 
Nilikuwa sijasikia huo wimbo

Dah.... Ninamkubali dogo, ila kwenye huu wimbo kazingua
 
umenena mtoa mada, young killer nyimbo za mchirilu awaachie akina dogo janja&young dar es salaam.
 
Chachasteven,

Fans bwana!

They think they can demand and pass judgements ruthlessly to their fellow humans about what they do!

Ni sawa lakini!

Hayanihusu,thats big real estate for nigga like me to be in!
 
Back
Top Bottom