Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Jaribu Kufikiri,
Umehangaika kutafuta business opportunity kwa njia unayoifahamu wewe,ukatafuta mtaji,ukaajiri wafanyakazi ili mfanye kazi pamoja mjenge kampuni,mjenge maisha.Ila Kila mara unajikuta unahisi kuna kitu unakikosa katika katika timu yako.Kuna wakati unafikiri labda hawana uzoefu au elimu au ujuzi wa kutosha.Kuna wakati unafikiri labda unawalipa kidogo sana au unawalipa kiasi kikubwa sana.Kuna wakatiunafikiri labda umekosea katika kuwaajiri.
Kuna mambo mengi sana ambayo unaona hayako sawa lakini bado unaona huna suluhu nayo.Unatengeneza Pesa na faida laini bado unaona kuna jambo haliko sawa.Hii ni moja kati ya changamoto ambayo wanapitia wafanyabiashara wengi wakubwa na wadogo.Swali la kujiuliza Je suluhisho yake nini?
Katika mazungumzo yangu marefu na mmoja wa wamiliki wa kampuni kubwa katika jiji la arusha ambaye naye anapitia changamoto kama hiyo niligundua tatizo ambalo linaweza kuwa chanzo cha hii changamoto.
Wajasiriamali wengi na wamiliki ya biashara hufanya makosa katika kuajiri wafanyakazi wao.Wengi wao husahau kwamba wafanyakazi wao nao ni watu ambao nao wana maono,malengo na mataraji katika maisha yao na kwamba wanapokuja katika kampuni au biashara yako wanataraji waweze kufikia malengo yako kupitia fursa unayowapa.Huwa wanasahau pia kwamba unapoajiri mtu basi lazima uwe na hakika majukumu yake yatakuwa ni yapi na yawe wazi na ya hakika na sio kuajiri mtu kwa ajili ya kujaza nafasi katika ofisi yako.
Wajasiriamali wengi huona raha kwamba watu wanaripoti ofisini mapema hata kama hakuna kazi za kufanya na wanakaa ofisi siku nzima hata kama hawana cha maana wanachofanya.Tunapoajiri tunanunua muda wa mtu ingawa hatuuhitaji muda huo.Tunasahau kwamba ajira sio muda tu bali ni zile skills za mtu ni sehemu ya ajira na ni lazima ufahamu namna ya kuzitumia.
Lengo la kuleta mjadala huu ni kutaka kujadili mbinu ambazo unaweza kuzitumia kujenga timu ya wafanya kazi wake na kuifanya iwe na tija kwako na kwenye biashara yako.Je utazame vigezo gani wakati wa kuamua nani umuajiri?Ni vigezo vya msingi vya kuzingatia katika kufanya uamuzi wa ni nani aajiriwe katika kampuni yako na kwa nafasi gani?
Karibu tujadiliane