Tanzania Tech
JF-Expert Member
- Dec 8, 2016
- 355
- 276
Naona kama bado hakuna mtu anafahamu kuhusu ili so nimeona nianzishe uzi kuhusu ili ili kusudi watu wote wafahamu kuhusu mabadiliko mapya yanayokuja kwenye mtandao wa YouTube. Kama wewe ni mmoja wa watu wenye channel na upo nje ya marekani basi hii ina kuhusu kwa asilimia 100.
Kuanzia mwezi wa sita mwaka huu 2021, YouTube inategemea kuanza kukata kodi kwenya mapato yote yanayotokana na watazamani wa wanao angalia video zako kutoka nchini marekani. (Kama unavyojua marekani ndio inachangia mapato makubwa kwa creators wengi hivyo hii lazima inakuhusu na itapunguza mapato yako kwa namna moja ama nyingine). Sasa kutokana na hili YouTube inakutaka kutuma maelezo ambayo yataweza kutathimini kiasi cha kodi ambacho unatakiwa kukatwa kila mwezi.
Bila kufanya hili kabla ya mwezi wa sita mwaka 2021, utakatwa hadi asilimia 24 ya mapato yako yote bila kujali kiasi kichotokana na watazamaji wa marekani au lah. Sasa ni muhimu kujaza fomu hiyo sasa kwani fomu hiyo kama haijazwa mapato yako ya mwezi ambayo hufanyika tarehe 21 kila mwezi yatasitishwa hadi utakapo jaza fomu hiyo.
Unaweza kuanza kujaza fomu hiyo kwa kuingia kwenye akaunti yako ya Google Adsense na kuanza kujaza fomu hii haraka sana. Kitu unachotakiwa kujua ni kuwa kuna pande mbili kwenye hili, wakati wa kujaza fomu hii utaulizwa kama nchi yako inayo Tax Treaty na marekani na kama haina basi jiandae kukatwa hadi asilimia 30. Nimesaidia watu kadhaa kujaza fomu hii na asilimia zinazo chukuliwa ni asilimia 30 kwa Tanzania kwa sababu Tanzania haina Tax Treaty na Marekani. Unaweza kupata maelezo kwa kuangalia nchi zenye Tax Treaty na marekani hapo chini. Au tembelea tovuti ya IRS ya marekani hapa.
Angalia kwenye sehemu ya Copyright kujua kiasi au asilimia ambazo unatakiwa kukatwa. Kama unavyoweza kuona kwenye list hapo juu Tanzania haipo hivyo inabakia kwenye sehemu ya mwisho ambayo ni Other Countries ambapo utakatwa asilimia 30 ya mapato yako unayo yapata kutokana na viewer wako ambao wana angalia video zako na kuona matangazo kutoka nchini Marekani.
Hapo chini ni moja ya mtu ambae nime msaidia kusubmit hiyo fomu na moja kwa moja inakuja asilimia 30, hii ni sawa na kusema kuwa asilimia hiyo itakuwa inakatwa kwenye kila mapato yanayo tokana na views kutoka nchini marekani.
Hii ni sawa na kusema kuwa kama ulikuwa unapata dollar $100 kutokana na viewer wako kutoka nchini marekani asilimia 30 ikiondolewa kwenye hiyo $100 utabakiwa na $70, hivyo ni muhimu kuangalia ni kiasi gani cha pesa unacho tengeneza kutokana na view za watu wa marekani kisha utoe asilimia 30 ili kupata ni kiasi gani kitakacho katwa. Unaweza kuangalia video hapo chini jinsi ya kuangalia kiasi cha pesa unachopata kutokana na viewer wa marekani.
Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma zaidi hapa
Naomba kuwasilisha kama una maswali unaweza kuuliza kupitia hapo chini maana hii mada iko deep sana.