YouTube Yaja na YouTube story/status

YouTube Yaja na YouTube story/status

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Mtandao wa YouTube unao milikiwa na Google waja na YouTube story.
Youtube story ni kipengele cha kumruhusu mtumiaji wa YouTube mwenye account yaani youtuber kuweka hadithi kama ilivyo mitandao mbalimbali ya kijamii mfano Facebook na Instagram wao pia wanatumia Facebook story au instagram story pamoja na WhatsApp yenyewe ikiwa na WhatsApp status.
Mtandao huo utamuruhusu youtuber kuweka story na watumiaji wengine wa mtandao huo wao watakuwa YouTube story viewers.
Lakini utofauti wa YouTube story na mitandao mingine ni kwamba mitandao mingine story/status zake hupotea kila baada ya masaa 24. Lakini YouTube yenyewe story hiyo itapotea baada ya wiki 1.
Kwahiyo mtumiaji ataweka hadithi yake na kutoweka baada ya wiki 1 (masaa 168).
Faida moja wapo ya kuweka YouTube story kwa mtumiaji ni kuwasaida Wafuatiliaji wake kujua kama account hiyo bado ipo Active kwa YouTube channel ambazo haziwezi maudhui mara kwa mara.
NB: kwa sasa YouTube story itaonekana kwa subscribers tu.
 
Ina utofauti na YouTube shorts?
Ndio mkuu.
Youtube shorts zenyewe vinakaa mda wote mpaka utakapo zifuta, pia kama YouTube yako unalipwa hata YouTube shorts wanajumuisha.
Lakini YouTube story zenyewe zinatoweka baada ya wiki 1 yaani kama status za WhatsApp zinazo kaa 24hrs, pia YouTube story hazilipiwi na YouTube kama channel yako inalipwa.
 
Kwahiyo hii basically ni faida kwa YouTube zaidi, wengine labda watumie kwa matangazo
 
Back
Top Bottom