Nimelazimika kuandika uzi huu baada ya kukisikia kibao cha "Kasongo" kikirindima.
Nimemkumbuka mtangazaji huyu aliyekuwa mwahiriwa wa RFA kipindi mahsusi kikiwa salamu za milenium (Nyimbo za zamani zilizopigwa mpaka ikavuka soksi na kiatu kubaki pale pale) na star tv kipindi cha roving dj,
Kwa hakika alikuwa mkali sana huyu jamaa, alikuwa anavimudu vipindi vyake.
Kokote alipo Namsaluti kwa saluti ya askari wa kinazi.
Hivi yupo wapi siku hizi na anafanya nini manake hatumsikii kwenye maredio wala matiivii.