Yuko wapi Kayumba?

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,415
Reaction score
119,473
Heshima kwenu wakuu..
Mara nyingi huwa najiuliza hivi yule mtoto alikuwa anaigiza kwenye vibonzo vya Hakielimu yuko wapi siku hizi? Mtoto alikuwa na kipaji cha kuigiza sio cha nchi hii na kupitia yeye hizi shule za sisi walalahoi zilibatizwa jina la St. Kayumba....nadhani anaweza kuwa amemaliza hata chuo.
Kile kipaji kilitakiwa kiendelezwe manake mtoto alivyokuwa anajua kuuvaa uhusika utasema ndio maisha yake.
Natamani nimuone kwa kweli...ukitupia picha yake sio mbaya ( ni celebrity yule kwa hiyo kutupia picha yake haliwezi kuwa kosa)
 
Mimi nikajua kayumba wa m50 za star search.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…