Yuko wapi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman?

Yuko wapi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman?

Kiokote

Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
86
Reaction score
42
Ni kitambo kidogo tangu kiongozi huyu aonekane hadharani. Ni zaidi ya miezi karibu 7 Mhe. Othman hajaonekana kwenye tukio lolote la Kitaifa.

Mfano ni hivi karibuni Masoud hakuwepo Dodoma katika Hafla ya Uzinduzi wa Ikulu ya Chamwino. Si hivyo tu, hata kwenye matukio makubwa ya Kisiasa visiwani Zanzibar bwana huyu hajaonekana.

Naomba kuuliza, Je, yu mgonjwa? Kwanini Chama chake kiko kimya? Nakumbuka wakati ule JPM haonekani hadharani Zitto Kabwe na wenzake walipaza sauti kutaka ifahamike aliko kwasababu suala la afya ya Kiongozi wa Kitaifa sio siri. Je, si muda muafaka Zitto na ACT watoke kutuambia aliko ndugu Othman. Au tuamini hali si shwali ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa SMZ?

Naomba kufahamu.
 
Back
Top Bottom