Yuko wapi Mohamed Hussein Mmachinga?

mdogo wake anaitwa FIKIRI HUSSEN MMACHINGA na dada yao pia wote walikuwa wachezaji wazuri tena vipaji hawa wadogo zake ni mapolisi ccm pia omari husseni huyu alikuwa majimaji ile ya garincha
Naipata Sana hii familia na sifa yao kuu watoto wote wa kiume wana miguu yenye tege la nje(miguu ya kushoto)wanapiga sana mpira hawa watu isipokua yule jamaa Shaibu Hussein amejikita kwenye udereva,baba yao(mzee daima) ni mnazi mkubwa sana wa yanga ila ni nguli wa ndumba hatari,kipindi cha shule shule kuna mdogo wao mmoja hivi aitwa Tatu Hussein teh teh teh nyumbani kwao ni pale mtwara karibu na polisi kotaz jirani na kwa masawe Ukimuona msalimie mwambie Chinga One wa jf anakusabahi sana.

Nimepamiss sana mtwara,hivi john Mental yupo?
 
Reactions: BRN

Hivi Mohamed Hussein na yeye ni Yanga Damu? Niliumia sana alivyo enda simba hiyo mwaka 2001.
 
Hivi Mohamed Hussein na yeye ni Yanga Damu? Niliumia sana alivyo enda simba hiyo mwaka 2001.
Family legacy,full yanga kuanzia babu mpk mjukuu.sema kwenda simba alikua kazini anasaka mpunga.
 
Family legacy,full yanga kuanzia babu mpk mjukuu.sema kwenda simba alikua kazini anasaka mpunga.
Nimefurahi kusikia hivyo coz nilikuwa namkubali sana Mmachinga. Hata ishu ya kwenda Simba ilitokea kimagumashi tu, mpango ulikuwa asajili Moro United, ikatokea bahati mbaya baadhi ya matajiri wa Moro United walio husika na kumsajili, ni Simba Damu, wakaamua kumpeleka Simba
 
Ahaa naona na wao ni familia ya kandanda kama kina Julio. Omary Hussein anachezea chama gani?
Atakua veterani now ila alishachezea Bandari Mtwara,Simba na Majimaji
 
Mohamed hussein kwa sasa ni kocha anaekinoa kikosi cha soka toka timu ya wafanyakazi wa FINCA Microfinance Bank . huku pia akijishughulisha na kazi zake nyingine. Mara kadhaa anaonekana katika viunga vya TAN HOUSE Victoria yalipo makao makuu ya benki hiyo.
 
Nilikuwa namkubali sana huyu striker wetu wa Dar Es salaam Young Africans..Tanzania hatotokeaga striker mwenye ubora kama Machinga
 
Nilikuwa namkubali sana huyu striker wetu wa Dar Es salaam Young Africans..Tanzania hatotokeaga striker mwenye ubora kama Machinga
mashuti makali ya chini yanayolenga lango,na anapiga huku anakimbia
 
Family legacy,full yanga kuanzia babu mpk mjukuu.sema kwenda simba alikua kazini anasaka mpunga.
Hata kwenye mechi za simba veterans vs yanga veterans anachezeaga Yanga. Kifupi wana jangwani bado tunamtambua kama shujaa wetu
 
Alitibua historia yake kidogo alivyochezea simba, ila Chinga one kilikuwa kipaji halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…