mbotoki
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 268
- 115
Bhule bhule bhakamu gwangu.
Nikiwa kama mdau wa michezo, hususan Mpira wa Miguu, ninafurahi sana kuona Kwa siku za usoni, "jinsia" inachukua sana mkondo wake, haswa kwenye mchezo huu wa kabumbu. Lakini napenda kujikita zaidi hapa nyumbani.
Ninafurahishwa sana na hali ilivyo siku hizi, nikifuatilia mchezo huu naona unazidi kuwa mchezo pendwa kwa wananchi jinsia zote.
Siku hizi ukiingia viwanjani mashabiki tu ni karibu tunagawana kwa upande wa jinsia. Yaani utakuta idadi ya wapenzi, washabiki, wanazi, wanachama wa time yao pendwa Karib wako nusu kwa nusu ki gender.
Tumefika Mbali zaidi, hata katika baadhi ya team hizi za kambumbu, mpaka safu za uongozi za baadhi ya team hizi utakuta wake kwa waume wako safuni.
Sasa huko likaenda Mbali zaidi mpaka sasa kwenye safu za uamuzi, yaani katika mchezo huo, kuna waamuzi wakinamama, ambao wanafanya vema sana wanapokuwa majukumuni.
Mfano huyu Dada yetu Mwenyewe "beji" ya FIFA ajulikanaye kama Joanister Rukya.
Huyu binti kwa kweli anajitahidi.
Sasa nikirejea kwenye mzizi, wakati huyu akianza kuchipukia katika uamuzi, alikuweko mwingine ambaye naye alikuwa moto wa kuotea Mbali, Mwamuzi aliyefahamika kwa jina la "Judith Mbaga"
Huyo naye aisee alikuwa anamudu mikiki ya ligi yetu juu ya hapa bongo, yaani alikuwa kichezesha, mdau unakuwa hauna hata tone ya shaka ya maamuzi.
Binafsi nilitarajia angelifika Mbali sana, ukizingatia alikuwa akienda mpaka nje kuchezesha mashindano mfano ya awali ya Klabu bingwa Afrika.
Ilitokea tu akayeyuka vuuup, aisee, hili ndo limenifanya niandike hapa, mwenye kufahamu alipo jamani Mwamuzi huyu hebu nipe data.
Yuko wapi?
Anaendelea na uamuzi?
Amefikia level gani ya uamuzi?
Kweli alihamasisha sana hata wale nilisoma nao mpaka wakatamani kuwa kama yeye.
Sasa wanamuulizia nami jibu sina.
Amaan iwe nanyi.