Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Miaka ya 2000 nakumbuka kipindi hicho Sheikh Nurdin Kishk alikuwa kiboko ya bidaa basi nikawa napenda sana kuangalia kanda zake. Siku hiyo kwenye 2008-2009 nikaenda Dar kurudi nikarudi na cd za mafungu za kutosha nikawa naangalia kwa kina fulani ambaye ni rafiki yangu wa damu
Miongoni mwa kanda zile ambayo siisahau ni ya Mzee mmoja kutoka Mkuranga ambaye alikuwa akidai kuwa anashushiwa wahyi kutoka kwa mwenyezi Mungu. Sheikh Kishk kama kawaida na jopo lake wakatinga kwa Mzee yule ili kufanya nae mnakasha. Basi bwana Mzee Abdallah Salum pamoja na maswahaba zake ilikuwa ni kichekesho sana
Nasema kichekesho kwani kwa namna mashekhe wale walivyokuwa wamejiandaa na walichokutana nacho binafsi niliona ni vitu viwili tofauti kabisa. Mzee na watu wake walikuwa ni watupu kabisa na hata walipobananishwa warejee vitabu hayupo aliyetoa andiko zaidi ya porojo tu. Mzee anavyoongea tu unaona hakuna anachosimamia bali mashetani tu yalikuwa yamemchezea
Vitu vilivyonifanya nicheke sana na kuipenda ile kanda ni kwanza mzee mwenyewe, pili kijana mmoja ambaye alikuwa mjanja janja sana muongeaji na tatu ni kina kishk na jopo lake walivyokuwa wakitumia busara ya hali ya juu sana kuzungumza na wale watu. Video ile ndiyo ikanifanyaga nione kazi ya uhadhiri wa dini si lelemama.
Nilifuatilia sana enzi zile kama ningeona CD ya mwendelezo wa wale watu kilitokea nini baadae lakini sikupata. Sasa juzi katika kuzurura YouTube si ndio nikakuta zile video tena kwa bahati mbaya zikiwa vile vile hazijaendelea.
Nikajaribu kutafuta taarifa bila mafanikio ndomaana nikapata wazo la kuuliza humu kama kuna mwenye video nyingine kuhusu yule mzee na vijana wake au mwenye taarifa hata ya mdomo tu kwamba wale watu ilikuwaje aniambie. Maana mashekhe waliazimia kurudi mara nyingine na watu wale walionesha wapo tayari kwenda kusoma nje na kwa Mzee Abdallah Salum. Natumai taarifa zao kuhusu mbeleni walivyokuja kuwa ni nzuri sana bila shaka hususan yule kijana (m'baba) muongeaji sana