Unaonyesha una matatizo ya akili ,huna wazimu lakini ni mfinyu wa kupambanua na kuyaelewa mambo kwa undani halafu ukayakubali ,watu dizaini zenu ni wale ambao mnakumbwa na kufagiliwa na fagio la propaganda ,mnanunulika kirahisi kwa maneno ya kuchonga ,na yakishawaingia katika akili yako inakuwa ni itikadi kwa upande wako hivyo inamuwia vigumu mtu kukufahamisha kwani inakuwa tayari kasumba imeshajengeka.
Kwa ulivyoleta mambo ya Jumbe na kuunganisha na Seifu ndipo nilipokubaini ni mtu unaekokotwa na propaganda pengine kama ungeendelea kuhubiri ungelisema Seifu anataka kuleta waarabu ,inaonyesha hujui siasa zinavyokwenda na unashindwa kuelewa maana ya watu kusema siasa ni mchezo mchafu.
Halafu nimekugundua kuwa ni mchovu wa kufikiri kwa kung'ang'aniza mambo yalioibuka kisiasa ,unajua wakati wa vita kuna nyimbo nyingi zinazuka na vita ikimalizika ,na hizo nyimbo nazo husita ,ila wewe bado unaziimba wakati vita ilishakwisha sasa sijui kwa miaka hii tuliyonayo kama nyimbo za wakati huo zitakusaidieni.
Umemsikia Muhunzi akisema anamtambua karume kama Raisi wa Unguja ,hivyo wewe kama mfuatiliaji na mtu unaweza kufikiri ,ulitakiwa ujue hiyo ni nyimbo ya vita nyengine imeanza ile ya kutomtambua Raisi imeshapitwa na wakati.
Using'ang'anie mbona walisema hawamtambui ? ndio mfano wako unaleta mambo ya Jumbe ,ndugu elewa kuwa watu hawazungumzii somo la historia hapa kuna siasa ambayo inabadilika kwa nyakati.
Jaribu kutafuta hoja nyengine mpya kabisa za Jumbe hazitokusaidia kitu ,kwani haiwezi leo tukaingia vitani na Kenya tukamwita Kibaki nduli bali tutamtafutia jina jingine jipya linaloendana na wakati ,si umiona wahujumu uchumi sasa wanaitwa mafisadi ? yaani nakushangaa sana unaleta mambo ya Jumbe na Seifu na uarabu na udini au ualkaeda yaani nyimbo za uchaguzi za mwaka juzi na zaidi unakuja kuhadithia leo.Ndio nyie nyie mnaokazania Zanzibar wana historia ya mipasuko ,ila kumbuka tu siasa ya vyama vingi ilianza Zanzibar kuliko Tanganyika ,hivyo kwenye vyama vingi hakuachi mipasuko ,seuze ndani ya chama kimoja si tunaiyona CCM si imejaa mipasuko ambayo ukitazama unaona mpaka ndani.