Yuko wapi Raila Odinga wa Tanzania?


Mavanza;

Mkuu, hakika umenena, umenena muungwana, kweli ni lazima wengine wetu tujitoe kafara kwa faida ya kizazi kijacho, haiwezekani Mafisadi wazidi kuneemeka huku hatima ya watoto wetu haijulikani, haiwezekani mitoto ya mifisadi ndiyo iifaidi nchi hii, haiwezekani ndugu yangu, ila tutampata wapi Raila wa nchi hii?
 

IsayaMwita, USITAFUTE MKOMBOZI! Jikomboe. That is my message.
Raila Odinga is not a hero to everyone, kwa other Kenyans he is the deivl personified. Kwa hiyo usitake kutafuta mtu mmoja. Angalia dynamics and the environment. Tujenge pamoja taifa inayofuata sheria na inayofuata misingi ya haki za binadamu.
Hatutampata Raila Odinga au Obama au whoever tunamtafuta, because tunahitaji weneywe kufanya mabadiliko then a leader will eventually arise ambaye atatusikiliza sisi na kutusaidia kujenga. Usitake mtu aibuke na aje na mawazo how to do it. Watanzania sisi siyo watoto ni watu wazima, we are thinking people and we know what we want nd what to do. Tatizo viongozi wetu wamekuwa wakitu-treat kama watoto wadogo.
 

Susuviri;

Tunapoongelea mtu anayeweza kufanya mabadailiko ndani ya taifa letu, hasa hulenga wale viongozi wenye mitizamo chanya, napenda kukuuliza swali kidogo tu, hebu mtu kama wewe wawezaje kujikomboa(kisiasa)? usisahau kuwa hata diwani wako hakujui, sasa wawezaje kujikomboa? ndipo nikabainisha kuwa kuna kila haja ya kuwa watu(viongozi) wanaoweza kutukomboa na si vinginevyo,

Nadhani uongozi na fikra zenye tija katika jamii zinahitajika, sitegemei mtu yeyote kusimama na kuweza kujikomboa hasa kisiasa, ni ngumu kama nikel, tuwe na mwelekeo na kuendelea kuwashawishi wale tunaodhani kuwa wakisimama na CCM wataleta changamoto na si vinginevyo.
 

Isayamwita,

Obama alikuwa nani miaka mitano iliyopita na sasa yuko wapi? Mtu kama Zitto alikuwa nani miaka mitano iliyopita na sasa yuko wapi?

Timiza wajibu wako na kuna siku Tanzania itakuja pata kiongozi wa maana.

Viongozi hawatoki mbinguni, tunao kila siku. Mazingira ndiyo yanawafanya wengine wafanikiwe kuwa viongozi bora wakati wengine wanaporomoka. Endelea kujenga mazingira bora ambayo ni kujituma, kufuata sheria na haki.

Kwa mazingira ya sasa ya Tanzania, hata tukimpata Odinga wa TZ, hatafanikiwa maana atatimuliwa na kupotea baada ya muda mfupi. Ukisoma kashfa na matusi wanayopokea watu kama akina Mrema hapa JF, juwa sisi wananchi bado hatujawa tayari kuwaunga mkono watu ambao wamejitolea maisha yao kupigania haki. Hata Odinga sawa na Mrema, ana makosa yake mengi tu, ila Wakenya wamemkubali kwasababu wanajua pamoja na makosa yake kama binadamu lakini muda wote kajitolea kusaidia kuleta ukombozi wa kweli wa Kenya.

Mazingira ya siasa za Kenya na Tanzania ni tofauti sana.
 

Mtanzania;

Hakika mtanzania umenigusa, umenikuna Mkuu, kweli watu kama akina zitto,Slaa hatujui kesho watakuwa nani katika taifa letu, pia ninazidi kuwashangaa watu wanaoweza kuwatukana watu kama akina Mrema, hakika watakuwa hawawatendei haki.

Mtanzania; ila jambo ninalotaka kutofautiana na wewe ni kwamba eti kwa sasa mazingira ya siasa za Tanzania hayaruhusu mabadiliko mimi naona hiyo si kweli, nadhani labda viongozi wetu wa kisia sa hawajaamua kuwa nadhamira ya dhati tu, je utakumbuka kuwa kwa sasa bunge kwa kupitia wabunge wachache wa upinzani wameweza kuleta mtizamo mpya wa kifikra ndani ya nchi yetu?

Wakati umefika tukaze kamba, hawa CCM hakuna siku watakubali demokrasia ya kweli hapa Tanzania hata siku moja ni wakati wetu sasa sisi wanyonge kujipanga, kwani hawa mafisadi watazidi kujiimarisha na pia kujiweka nafasi nzuri ili kuitokomeza hii Demokrasia changa inayoanza kuibuka hapa Tanzania.
 

Naona unaota ndoto za mchana ndugu na hizi nadharia zako zisizo na mguso wa hali halisi duniani. Hakuna jamii ya binadamu iliyoweza "kujikomboa" yenyewe bila kuwa na kiongozi hodari, shupavu, mwerevu mwenye abundance of both moral integrity and dignity of character. Jamii ya watu haiwezi kujikomboa tu kila mtu kivyakevyake bila mwelekeo unaoleweka na mtu wa kuongoza mapinduzi. Raila siyo "mtakatifu" na hakuna anayedai kuwa hiyo ni necessary au sufficient requirement ya kuwa kiongozi mzuri. Hakuna anayetegemea Raila awe shujaa kwa wote lakini kubali usikubali kwa walio wengi hiyo ni sifa moja kuu aliyo nayo Raila.
 

Njabu Tha Dude;

Mkuu hakika acha utani, hapa tunajadili hoja na si mzaa , kweli unataka utuambie kuwa hakuna mtu mwenye fikra njema kama za Raila hapa Tanzania? kweli sisi sote hatuna fikra za kimapinduzi kama za Raila? nadhani sisi fikra hizo tunazo ila uoga na upumbavu umetujaa na si vinginevyo,

Swali dogo naomba ulijibu hapa, je akina Slaa,Mwakyembe, anna kilango , na hata Zitto si mfono wa Raila?
 

Naona hapo kwa kiasi kikubwa ushajijibu mwenyewe. Tatizo si kukosekana "fikra za kimapinduzi", bali ni historia ya kisiasa ya nchi haichangii kuleta kiongozi wa upinzani mwenye wasifu aliyonao Raila. Hao uliowataja kwa pekee yao hawana mvuto mkubwa wa kisiasa kama aliyonao Raila na sidhani kama wanaweza kupata mamilioni ya wafuasi waliyo tayari kumwaga damu ikiwezekana kutetea haki zao. Watu kama Slaa na Zitto wana potential lakini hawawezi ku-achieve mabadiliko makubwa kama alivyoweza Raila.
 

Njabu Tha Dude;

Kwa kuwa sisi watanzania hatuna tamaduni za kujitolea muanga, ila ninachodhani kama tunaweza kujijenga na kujiamini sisi kwanza(wafuasi) hakika zile nidhamu za uoga zinaweza kututoka, tuna watu wa kutolea mifano, watu toka Mara ni watu wa mfano huo, tunaamini hata watu toka kigoma pia wanaweza kuwa na mfano huo,.

Kuhusu hawa Viongozi tulionao wanaweza kusimama kama tutawaunga mkono, Mtu kama Slaa, akipata support anaweza kufanya kitu na jamii ya kitanzania ikapona na hii mikono ya mafisadi, ama wewe unaonaje?

Tatizo lililopo hapo ni kwamba Katika inchi yetu hairuhusu mgombea (binafsi)huru, na kama ndiyo hivyo je pale CHADEMA Mbowe anaweza kupisha uwenyekiti ili tumuweke mtu mfano wa Raila? hapo mnapaonaje?
 

Naona umesahau kwamba binadamu wote kwa asili wamezaliwa na "herd mentality". Bila ya kuwa na kiongozi jamii ya binadamu haiwezi kupata maendeleo yoyote ya maana. Umepoteza muda mwingi sana kuwajadili na kuwachambua Clinton, Obama na McCain, kwa nini? Mbona hukuishia kuandika waraka au kuhubiri injili yako ya jinsi Mmarekani wa kawaida anavyoweza "kuijkomboa" mwenyewe bila ya kuwategemea hao viongozi vinara wanaowania Urais?
 

Njabu Tha Dude;

Nashukuru sana kwa mtizamo wako na fikra zako njema, hapa tunajaribu kuona ni jinsi gani ya kujinusuru na na mikono ya hawa mafisadi, sasa mimi kama mimi nikawa nadhani ni kanjia gani kanaweza kutuponya na hawa mafisadi, chukulia mfano wa panya ndani ya nyumba, mara anakurupuliwa, panya yule atafanya kila njia ili aweze kujinuru na si vinginevyo, kwani akichelewa basi hapo atashambuliwa hadi umauti umfike.

Njabu Tha Dude;najua unaweza kuwa na jibu lenye tumaini, wewe kama wewe unadhani tuanzie wapi? usisahau kuwa muda nao unajongea!!
 
...........raila has explenary record and history..hapa nyumbani hakuna ..kwani wapuinzani wengi wa nyerere kama kambona.,mtemvus,kunambis ets ..walikuwa seized kisiasa na wala hawajaproduce offsprings wakali kisiasa...tanzania hakuna strong political family ninayoona zaidi ya karume na ali hassan mwinyi....nyereres hawafurukuti labda tungojee kizazi chao cha pili..hiki cha kwanza cha kina makongoro ..hakifurukuti unlike karume,mwinyi,kenyattas,railas ets....

ila tanzania kuna mwanasiasa kama JOHN POMBE MAGUFURI huyu ni admirer wa raila...na hopeful siku moja atafika mbali.....
 

issayamwita

Nadhani hili la ukabila ni kati ya socio-political dynamics ambazo zinafanya siasa za Kenya zitofautiane kimsingi na za Tanzania. Raila political base yake kubwa ni Waluo na Waluhya ambao kihistoria wamekuwa na upinzani mkubwa wa kisiasa na Wakikuyu. Tanzania haina siasa za ukabila, na ndiyo ndiyo maana wanasiasa kama Slaa na Zitto kamwe hawawezi kupata ufuasi kama aliyonao Raila. Labda kwa kiasi fulani Mpemba Seif Hamad jinsi alivyoiweka Pemba yote chini ya miguu yake kisiasa kila wakati wa Uchaguzi mkuu, lakini tatizo ni kwamba hana broad appeal inayojumuisha Wapiga Kura ndani na nje ya Visiwani. Hiyo ndiyo challenge kubwa ya siasa za ukabila.
 

phillemon mikael

Mbona umekata tamaa namna hii Mkuu? mbona hauna matumaini ya kuishi? umewahi kufika Mara? umewahi kufika Tarime? nenda leo kaone, njoo uone mkuu wangu, uone kuwa hauruhusiwi kuvaa yale maguo ya kijani(CCM) sasa kama tungekuwa tumeanzisha fikra kama hizi katika mikoa kama 5 tungeweza kuleta mabadiliko,

phillemon mikael ni lazima tuwe na fikra za kiukombozi, acha kudhani kuwa CCM ndiyo kila kitu, na hatuwezi kuteswa na hawa mafisadi, tutafurukuta hadi mwisho, tunasema maisha yetu kwa sasa yatakuja mikonnoni mwa mafisadi, kufa kwetu sawa tu.

phillemon mikael kama mtu atashindwa kufanya mageuzi ya kweli hakika Tanzania Mpya haipo, lakini kama sisi sote tutaunganisha nguvu zetu kwa pamoja ukombozi wetu uko karibu,

phillemon mikael naomba ujiulize nini hatima yetu katika Taifa letu, nini hatima ya watoto wetu kama kila kitu mafisadi wanagawana?
 

Njabu Tha Dude

Mimi kama mimi naona siasa za Tanzania bara ni nzuri kama tutawapata viongozi wa kisiasa wanaouzika, tatizo ni kuwa viongozi tulionao ndani ya vyama hawauziki, lakini kama tunaweza kuwapata viongozi wenye mitazamo mizuri kama Raila wa kenya kwa maana ya kuweka maslahi ya Taifa mbele hili linawezekana.

Njabu Tha Dude usisahau kuwa Raila amekuwa mbunge wa Rang'ata pale Nairobi kwa mihura kadha na pale si kwamba kuna wajaruo tu.

Njabu Tha Dude tunataka tumpate mtu(kiongozi) atakayeuzika 2010 na si vinginevyo. ama wewe hilo unalitazamaje?
 

issaya mwita...saluuti kamanda ..heshima mbele mkuu..unajua hadi leo najiulizaga zile asilimia 80 kiwete aliaipataga wapi wakati kuna mikoa kama ...mara,kigoma,mbeya .,iringa,kilimanjaro...est ambayo ina msimamo mkali...mimi naamini kwa miaka ya sasa hata mgombea ccm awe mzuri vipi ni vigumu kupata asilimia 80 kama hakuiba kura...ushindi wa asilimia 65 hadi 70 ndio likely kwa mgombea mwenye mass support kwa hali ya upinzani ilivyo.....nadhani kadiri uelewa wa wananchi unavyoongezeka tutarudi kwenye mass support ya asilimia 40 to 45 kwa wapinzani mwaka 2010...nadhani mwaka 1995 tulikuwa na ratio ya 60:40.....

hali ya wapinzani kutoelewana ilielekea kupandikizwa na ccm ndiyo iliyoangusha nguvu kubwa waliyoanza nayo..mwaka 1995...wakati mrema alipokuwa na nguvu ya kuangusha mawee..

nafurahi kusikia nguvu ya uelewa ya wananchi wa mara...mara zote napenda hawa ndugu zangu kwani sio wanafiki ...ukianzia kwa mwalimu..pale alipoamua kumpigia chapuo paul ndobbo .baada ya ccm kuweka mgombea mbovu......sasa nguvu ya wana mara inabidi tuione tarime...

issa hali ikoje tarime ???...nasikia ccm wanajipanga kushinda ...hasa kutokana na propaganda za kugombanisha umoja wa wapinzani ambazo inaonekana wanaelekea kufanikiwa......
 

phillemon mikael;

Mkuu acha vituko, subiri uone awamu hii hapa Tarime tunaweza kuwaletea mwandishi wa habari kule Bungeni, naye si mwingine anaweza akawa Kichele Nyaronyo kama atapitishwa, sisi wanamara letu moja tu, unafiki kwetu mwiko na tutamtuma aje kutetea maslahi yetu na si vinginevyo.

phillemon mikael; Tunajua sisi wana Mara ndiyo chachu ya siasa hizi za Tanzania hii, Mwalimu alionyesha njia na sisi tunafuata, tutaweza kama mtatuunga Mkono

phillemon mikael; sisi sote tunaamini nchii ni yetu sote hakuna hata mmoja wetu anayestahili zaidi kuliko mwingine, nadhani sasa sisi Wana JF tuamke sote tuwaelimishe ndugu zetu kule vijijini tunakotoka.

phillemon mikael; kazi hiyo hapa Tarime tumeimaliza, sasa tunaelekeza nguvu zetu Msoma MJINI na mwisho Mwanza na kwingineko.

swali hili usilikwepe wewe kama wewe umeweza kuielimisha jamii unayotoka? jaribu sasa kuielimisha jamii yako Mkuu na hapo ndipo tutajikwamua na hawa mafisadi.
 

..nyoronyo kicheere huyu mpiganaji namkubali kwa sana.....kuna wakati walikuwa na mombare matinyi ofisi ikiwa ya majira pale karibu na club ya yanga...wakiwa pia na kiona mbali[conrad..]..it was a great team.....nilikuwa mara moja moja napeleka makalas....mara moja moja sana ....walikwa wakilipa kama sikosei tzs 10,000 miaka ya mwanzo ya 90...
 

phillemon mikael; sisi kama wana Mara tunataka kuonyesha umma wa kitanzania hata Waandishi wa habari bado wana nafasi katika uongozi wa Taifa hili sisi si wabaguzi hata Kidogo, tuna mtuma pale Mjengoni akatetee hoja zetu na si vinginevyo.

phillemon mikael; nimesema hii chachu itaanzia Mara, Tarime Lakini itasambaa Tanzania nzima , na CCM wajiandae na wakipenda Roho zetu wana mara halali yao, tutajitoa kafara kwa jinsi itakopohitajika.

phillemon mikael; Uwoga kwetu mwiko, maisha yetu mithiri ya makinda ya ndege, haiwezekani kamwe kuwaona watoto wa mafisadi ndiyo wanaoweza kusoma ,kuowa na hata kumiliki njia za uchumi, huku sisi tukiwa watazamaji.

phillemon mikael; si vizuri kufurahia hata kidogo kuona watoto wa maskini wakiteseka, wakikosa kalo, wakikosa matibabu ma hata kujifia kwa sababu ya njaa, tutapigana hadi kieleweke, ama wewe hilo unalitazamaje?
 

gagnija,

Pole sana kwa mtizamo wako huu, nadhani na wewe ndivyo mtizamo wako ulivyo na jinsi gani unavyoweza kudurusu mambo, napinda ufahamu kuwa Kenya imefikia demokrasia iliyokomaa na Raila ameiboresha kwa kiasi kikubwa, kwani ni yeye aliyeleta changa moto ndani ya taifa hilo.

Ni kweli kuwa Kenya kuna ukabila ila swala la demokrasia si swala la kikabila, mfano yule Raila amekuwa mbunge pale Lang'ata kwa muda sasa, nadhani sisi tusingependa tufike huko basi ni vema hawa viongozi wetu wa kitaifa kwa kupitia vyama vya upinzani wakalielewa hilo na kuacha kubomoana.

Laiti kama tusingekuwa na vyama vya upinzani hapa Tanzania hakika sijui ingekuwaje, sijui tungesemea wapi, sipati picha, labda tungeuzwa ughaibuni.

Eeee Mola Tulehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…