Yuko wapi Ramadhan Ally Kihiyo?

Nimemkumbuka sana wanajamvi Mh Kihiyo aliyekimbia ubunge Temeke kwa kuulizwa mwalimu wake wa darasa...Mwenye mawasiliano naye atujuze yuko wap Mheshimiwa??
 
Nimemkumbuka sana wanajamvi Mh Kihiyo aliyekimbia ubunge Temeke kwa kuulizwa mwalimu wake wa darasa...Mwenye mawasiliano naye atujuze yuko wap Mheshimiwa??
Kihiyo yupo anaishi Tabata Mawenzi-Dar; anaishi maisha ya ubabaishaji, anatapeli watu kwa kujiita Mbunge mstaafu. Ana skendo kibao za kiutapeli alafu ni miongoni mwa watu walioanzisha chama cha siasa kinachojulikana kama CHAUMA; anatembea na Briefcase ndani yake anajaza kadi za CCM na CHAUMA.
 
Ukibahatika kupata picha yake tuwekee hapa, kwani ni mtu muhimu aliyeongeza msamiati wa kiswahili-kihiyo" :asiyejua kitu; muongo, mbabaishaji etc
 
Nadhani ungemuuliza iwapo anajua kusoma maana alichouliza kipo kwenye post hapo juu
Ndio maana waliotuletea Elimu walituletea na Mitihani ya kufanya, maana jamaa kaeleza kila kitu ila kuna watu hawajamuelewa
 
Marehemu Mtopea alitokea tawi la NCCR la KWAZULU NATAR lililokuwa mtoni kichanga.
 
Lakini watu wengi wanadhani kihiyo inamaanisha mtu mwenye elimu ndogo, kumbe inamaanisha mtu aliyeghushi cheti kuonesha kiwango cha Elimu asichonacho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…