Yuko wapi Salum Shamte mwingine?

Yuko wapi Salum Shamte mwingine?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KHITMA YA SALUM SHAMTE TANGA: SAYYID MUHAMMAD HASHIM AMEULIZA, ''YUKO WAPI SALUM SHAMTE MWINGINE?''

Moja katika siku kubwa za kukumbukwa katika mji wa Tanga ilikuwa siku mamudir wote wa mji wa Tanga walipokutana nyumbani kwa Salum Shamte Bombo kuweka makubaliano ya pamoja ya kushikamana taasisi zao kwa pamoja kwa ajili ya Allah.

Leo nyumbani kwa Salum Shamte mbele ya nyumba yake ambako kwa miaka nenda miaka rudi toka Salum Shamte ahamie mji huo Waislam walikuwa kila mwezi wa Ramadhani watakutanika hapo mwezi wa Ramadhani patapigwa adhana na watu kufungua muadhini kwa pamoja na kufuturu pamoja kisha ikasomwa dua na watu kuagana, Waislam kutoka kila kona ya Tanga walikusanyika kwenye khitma yake na kumtakia maghfira.

Leo mchana baada ya visomo na dua alisimama Sayyid Muhammad Hashim akaeleza wasifu wa Salum Shamte juhudi alizofanya katika uhai wake kusaidia vyuo na taasisi za Kiislam akifanya yote kimya kimya akitia makazo mkubwa katika kusomesha dini kwa vijana.

Sayyid Muhammad Hashim akaeleza mengi jinsi Waislam wa Tanga walivyonufaika na maisha ya Salum Shamte katika umri wake wote alioishi Tanga.

Ndipo katika kuhitimisha maneno yake akauliza, ''Yuko wapi Salum Shamte mwingine?''

Picha ya kwanza aliye katikati akiangalia camera ni Salum Shamte na wa kwanza kushhoto ni Sayyid Muhammad Hashim wakati wa uhai wa Salum Shamte.
 
Nyie mnamjua Salum Shamte kwa mambo ya mkonge sie tunamjua Salum Shamte kama kiongozi wa Waislam."

Sayyid Muhammad Hashim

IMG-20200815-WA0070.jpg
 
Back
Top Bottom