Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Daah we jamaa umenifanya nimekumbuka mbali sana, enzi za akina Scandinavia, Ruvuma line, Tawaqal, Zainabu bus, safari ilikuwa fupi sana enzi hizo pamoja na kwamba muda wa kupanda na kushuka kitonga ulikuwa unakaribiana kutokana na hali upana wa barabara Kuwa mdogo johnthebaptist

Ukiachana na enzi za akina kiswele
 
Yule bwana alinitoa Mbeya saa 2 asbuhi na kunifikisha Dar saa 10 jioni, nilishilikia siti mwanzo hadi mwisho
 
Safina umesahau
 
Picha ngoja nimuombe mshana jr maana kwa zile mbinu zake lazima anazo!
Huyu Giriki nasikia alikuwa anatabia ya kuwaingiza wenzake chaka hasa wanaposhuka mlima Kitonga, yaani akishuka anamzuga wa nyuma yake kwa taa ili aone mlima mdogo mwisho wa siku wanyuma yake anashindwa kukontro gari anapata ajali' hii ni kweli au uzushi tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…