Yuko wapi yule jamaa wa ITV aliekua anasema kuishi Tanzania ni kupoteza muda tu

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,700
Reaction score
3,921
Kipindi cha nyuma kituo cha televisheni cha ITV kilikua kikirusha majadiliano ya wasomi wetu toka shule na taasisi mbali mbali za elimu ya juu, na tangazo kubwa la kipindi iki na lilikokua maarufu sana mwanzoni mwa miaka ya elf mbili, lilikua na jamaa aliekua anasema hivi:

"Umezaliwa Tanzania, umekulia Tanzania, ukasomea Tanzania, ukafanyia kazi Tanzania, wewe umepoteza muda wako wa maisha"

Naam, najua mtakua tu mmemkumbuka huyu jamaa, sasa ningependa kujua kama aliwai kufika tu ata Burundi au Kenya! Je yuko wapi Huyu?

Hii kauli mnaionaje wadau bado ina matter?

Najua miaka hii ya elf mbili kuja juu mambo ya video na TV hayakua makubwa kiasi icho, wengi walikwishaona au kuskia tangazo ilo maarufu.
 
Alitamka maneno hayo akiwa kidato cha sita makongo secondary kati ya 2001/2002 kwenye kipindi cha mgongano wa hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam, najua mtakua tu mmemkumbuka huyu jamaa, sasa ningependa kujua kama aliwai kufika tu ata Burundi au Kenya! Je yuko wapi Huyu?
Ungeweka picha yake ingekuwa vema zaidi mkuu.
 
Nadhani aliitwa kiomoni Kibamba wa Shule ya Makongo High School
 
Niko hapa, mnasemaj

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…