Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Leo nilikutana na Mzee mkongwe ambaye mara ya mwisho kuonana ilikuwa 2017, aliponiona akanichangamkia Sana huku akatabasamu, nami nilifurahi Sana Kwa maana huyu Mzee licha ya umri kusonga lakini akili yake bado ilikuwa na nguvu, baada ya kusalimiana Stori za hapa na pale zikaanza. Katikati ya Stori akaniuliza swali ambalo ndilo limenifanya niandike hapa.
Ati akasema; Taikon unachagua kipi Kati ya hivi; Nchi kupelekwa Kuzimu au nchi Kurudishwa Shimoni?"
Nikataka kumjibu lakini akanionya nisijibu Jambo lolote kwani Mimi bado ni kijana Mdogo, siruhusiwi kujibu maswali mazito Kama hayo.
Nikamuambia lakini nipo ndani ya nchi pia, akanisisitiza kuwa ninyamaze mpaka umri wangu utakapofika.
Sasa nikasema, Acha nije kuwauliza hapa,
Nchi kupelekwa Kuzimu au kurudishwa shimoni kipi mtachagua?
Majibu yatolewe na Watu wenye umri wa kujibu majibu Kwa maswali mazito.
Niliwaza labda ningemwambia Mzee Mkongwe kuwa nisingechagua Kokote iwe ni "KUZIMU" au "SHIMONI"
Lakini jibu hilo lingemaanisha kuwa ni kweli Mimi ni bado mtoto Kwa sababu nimemjibu jibu lisilokuwa limekusudiwa.
Wakubwa karibuni!
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa, Dar es salaam