Yupi anafaa kuolewa kati ya hawa?

DOGOSA

Member
Joined
May 22, 2012
Posts
8
Reaction score
1
Kuna kijana anahitaji ushauri wangu juu ya msichana yupi anafaa kumuoa kati ya hawa wawili anaodate nao, nimeona ni vyema kupata ushauri kutoka kwenu wadau kabla ya kumuadvice accordingly!

Binti wa kwanza ni mrembo wa haja - namaanisha mrembo kweli kweli, hawa wa kwenye magazeti tupa kule, ana elimu ya shahada ya kwanza kwenye mambo yetu yale ya uandishi wa habari. Anatoka familia bora - I mean mboga 7 na usafiri wa haja, that being the case anamuweka kijana mjini sana pindi anapopigika coz he is from familia zetu hizi za Mungu saidia siku zijongee. Tatizo binti ana sifa ya majidai na kuwadharau ndugu, jamaa na marafiki wa huyu kijana.

Binti wa pili ni mzuri wa kawaida sana na maisha yake ni ya chini coz wazazi wake hawana uwezo hali iliyopelekea kushindwa kupata elimu hata ya sekondari. Ila binti huyu ana upendo kwa watu wote na ni mchapakazi mzuri na anayejua kuhustle japo bado hajafanikiwa kuwa katika hali nzuri kiviiile!!

Huyu kijana alianza na binti wa pili, lakini alitokea kupendwa na huyu binti wa pili katika shughuli zake za kuuza nguo za wanawake kwenye kijiwe chake. Kwa hivyo jamaa anampenda binti wa pili lakini kutokana na maisha yake na mambo anayotimiziwa pamoja na ahadi anazopewa na binti wa kwanza anawekwa kwenye mtihani mkubwa maana anataka kuoa na wote wanasisitiza kuolewa, hapo chacha afanye nini wajameni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa hiyo, Huyo Jamaa mwenyewe anampenda binti wa pili na bado tunaombwa ushauri?
 
Achukue wa pili....huyo wa kwanza hata kama binti wa Bill Gates akawadharau wengine sio ndugu zangu :cool2:
 
Ndege wanaofanana huruka kwa pamoja! Tafakari, chukua hatua..
 
akili kichwani mwake... he is better placed to know which way he should go akizingatia future na uwezo wa familia yake
 

Hapo kwenye bold kasema wazi anampenda binti wa pili, nafikiri hilo ndilo chaguo sahihi. Binafsi sipendi na huwa sishauri vijana kukimbilia kuoa wanawake kwa sababu ya fedha na hali ya maisha waliyo nayo. Mwanaume aliyekamilika ameumbwa kutafuta pesa kwa jasho lake na kutunza familia yake akiwepo mkewe na siyo kupenda tabia ya kulelewa lewa kama binti, hiyo ni tabia mbaya.

Sioni pia faida ya yeye kuoa mke mwenye uwezo na ndg zake kushindwa kufika hata kumtembelea kwa kuogopa masimango, maringo na manyanyaso ya huyo mke mwenye hela. Ukitokea umepata mke mwenye upendo wa dhati na wewe unampenda kwa dhati na pesa anayo, then hiyo ni case tofauti na hii uliyoileta.

Ukiwa mwanaume ni vyema kujiamini na kutegemea maisha yako mwenyewe na siyo kulewa na fedha za baba mkwe! kuchapa Kazi kwa bidii, mipangilio mizuri na juhudi zako zitakupa maisha mazuri na heshima kuliko kuingia ktk hali ya kupoteza utu na uhuru wako na ndg zako kwa ajili ya pesa za mke. Kumbuka pia mapenzi si pesa, iko siku utamchoka na kujikuta umepoteza muda wako kwenye investment isiyo na returns ....

HP.
 
Mwambie achague anachoona kinamfaa kati ya kuoa au kuolewa
 
kila kitu kinatakiwa kianze kwenye point fulani sasa huyu hataki
kuanza kwenye point zero anataka akute kila kitu hii sio sifa ya kiume
amchukue binti wa pili kama anavyoona inafaa
 
mwambie ausikilize moyo wake. pili it seem mdada wa kwanza atakuja kumnyanyasa cos ana hela!
 
Dah mi naona ajitwishe huyo fukara, akitaka huyo wa familia bora itakula kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…