Yupi hapa yuko sahihi kwa dozi hii?

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,315
Wadau hamjambo?Nina vijana wangu wa kazi za shamba wawili.Bahati mbaya wote wana malaria na nikawapa hela wakanunue dawa.Bahati mbaya walikwenda maduka ya dawa tofauti.
Duka A. Mhudumu anasema mgonjwa aanze dozi saa nne kisha saa kumi na mbili asubuhi.Na dozi ya tatu atumie kama alivyoanza dozi ya kwanza yaani saa nne atafuatia saa kumi na mbili asubuhi hadi atakapomaliza
Duka B. Mhudumu amesema kama mwenzake kuwa aanze saa nne kisha saa kumi na mbili jioni.Dozi ya tatu anywe saa kumi na mbili jioni hadi anamaliza.
Je vyupi yupo sahihi?
 
Ndiyo "vyupi" yupo sahihi hapo. Unawaza nini pastor?
 
Duka B

8 hours then 12 hours hiyo especially kwa watoto

hiyo A pia huwa inatumika pia esp. kwa watu wazima
 

kwa ninimusingewapeleka hospital kwanza kuliko kwenda koja kwa moja duka la dawa??
 
Nadhani hiyo dawa itakuwa artemether/Lumefantrine(ALU).Kama ni hiyo then wote watakuwa wamekosea. 1st dose na 2nd dose lazima zipishane 8hrs. 3rd dose na kuendelea hupishana 12hrs-15hrs kwani Lumefantrine Ina half life ya 12-15hrs.:
 
A yupo sahihi. Dose ya pili ni masaa nane toka dose ya kwanza, na dose ya tatu ni masaa 24 toka dose ya kwanza, zinazofuata zinazofuata ni 12 hrly. Reference STG 2013

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…