Jamaa alikuwa anakata Tungi kuliko Mamba! Alipelekwa Mwanza kwenda kutangaza RFA kwa ndege, akauchapa usingizi ndani ya ndege kwa pombe walizokuwa wanapewa abiria, mtu aliyekuja kumpokea akarudi bila kumwona. Na kwa kuwa wahudumu wa ndege zetu hawako makini wakamstukia wakati ndege inarudi Dar ameuchapa usingizi. Ndipo ukawa mwisho wake. Alikuwa anapatikana maeneo ya Posta akipiga mizinga mpaka ya Mia tano. Pia alishajiingiza kwenye utapeli. Inasikitisha sana kupoteza kipaji kwa ulevi.
Ulevi ni nouma!