Yupo wapi Jose Chameleone?

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,822
Mwanamuziki huyu alivuma sana Afrika Mashariki kwa sisi ambao ni wahenga kidogo, miaka ya mwanzoni mwa 2000.

Alikuwa akitusuuza nyoyo zetu kwa vibao vyake vikali kama "mama Mia" "acha kulia mambo ya Dunia!"

Na vingine kadhaa kwa wakati ule Jose Chamilione na wadada waliokuwa wanajulikana kama obssesion walilikamata vema soko la Afrika mashariki.

Muziki toka Uganda Ulivuma ipasavyo.

Je, leo hii Jose Chamilion yuko wapi?

Au soko lake limemezwa na Diamond Platnumz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasasa Diamond amelishaka ipasavyo soko LA Africa mashariki. ktk nchi hizi tano, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, na Tanzania, sidhani Kama kuna mwanamuziki anaemfikia ktk kutoa burudani. Huko Kenya juzi wakishangaa jamaa ka paform jumla ya masaa matano bila kupumzika na kila ngoma Kali.

Wanasema tangia waijue dunia hakuna hata mwanamuziki mkenya aliepafom kwa muda mrefu hivo. bahati kama hizi ziliwatokea watu kibao tu lkn walizichezea akiwemo Juma nature, lkn naseebu kaitumia vizuri, hata akipolomoka Leo ki music hafi masikini.
 
Kuna wimbo wa Lady Jydee unaitwa "Historia" !! Sikumbuki vema maneno yake lakini huenda ni wimbo unaoishi.

Kwa kishindo alichokuwa nacho Jose Chamilione sikutaraji anaweza kupotea kirahisi hivi!

Huenda sisi wengine na wasanii wetu wana jambo la kujifunza hapo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa anaendelea na mziki na ana pesa ndefu. He was once ranked 10th of the most richest musicians in Africa.
 
Na wakati mwengine ni ile hali ya kutokua na mipango isiyokua ya kibiashara, sasa mtu amepata hela kdg tu anakimbilia kujenga ghorofa!!!!, investment za ki nssf hizo.
 
Mkuu kawaida ya muziki huwa unasikika. Ukifanya muziki hata kama ni chumbani kwako lazima majirani zako wasikie.

Kama anaendelea na Muziki je anaufanyia wapi? Au kazi zake anazifanyia sayari ipi?

Katika ulimwengu huu wa utandawazi tusingeshindwa kujua kama ana kazi yoyote ya muziki anayoifanya.

Usisahau hata Mr Nice Bado anafanya Muziki, Saida Karoli bado anafanya muziki.

Lakini Level zao kwa sasa si za wakati ule.

Ukisema ana pesa ndiyo huenda anazo lakini pesa huwa na kawaida ya kuisha na kupotea hatimaye mtu hufirisika!

Jamaa anaendelea na mziki na ana pesa ndefu. He was once ranked 10th of the most richest musicians in Africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Joseph Mayanja (anajulikana kwa jina la kisanii Jose Chameleone au Chameleone , wakati mwingine Chameleon; alizaliwa mwaka wa 1979) ni mwanamuziki wa hip hop na ragga kutoka Uganda . Yeye huimba hasa katika lugha ya Kiswahili.

Wasifu
Chameleone alianza wasifu wake mwishoni mwa miaka ya 1990, watengenezaji wake wa muziki wakiwa Ogopa Deejays kutoka Kenya. Moja kati ya nyimbo zake ya kwanza ilikuwa "Bageya", ikimshirikisha Redsan , msanii kutoka Kenya. Pia alishirikiana na mwananchi mwanamuziki mwenzake Bebe Cool, lakini baadaye iliiibuka kuwa wawili hawa walikuwa na upinzani mbaya.

Mtindo wa Chameleone wa muziki ni mchanganyiko wa muziki wa tamaduni wa Kiuganda[1], rumba ya Kati ya Afrika, Zouk na ragga. Albamu yake ya kwanza ilitolewa nchini Kenya mwaka wa 1999. Tangu wakati huo ametoa albamu kadhaa zikiwa pamoja na "Bageya" mwaka wa 2000, "Mama Mia" mwaka wa 2001, "Njo Karibu" mwaka wa 2002, "The Golden Voice" mwaka wa 2003, "Mambo Bado" mwaka wa 2004 na "Kipepo" mwaka wa 2005.

Yeye ni mwanachama wa Jamii ya Mwanamuziki, muungano wa wanamuziki ambao hutumia umaarufu wao na mali yao kusaidia kuondoa umaskini na kujenga kampeni za mwamko wa VVU / UKIMWI . Ametembelea idadi ya nchi za ng'ambo zikiwemo Marekani , Uingereza na Sweden miongoni mwa mengine.

Ndugu yake mdogo, anayetumia jina la kisanii la Weasel, ni mwanamuziki pia.

Diskografia

  • Albamu:
  • Bageya (2000)
  • Mama Mia (2001)
  • Njo Karibu (2002)
  • The Golden Voice (2003)
  • Mambo Bado (2004)
  • Kipepeo (2005)
  • Shida za Dunia (2006)
  • Sivyo Ndivyo (2007)
  • Katupakase (2007)
  • Bayuda (2008-2009)
Nyimbo zake kadhaa zilizoenea
  • "Jamila"
  • "Mama Rhoda" (ikimshirikisha Bushoke) [1]
  • "Shida za Dunia"
  • "Kipepeo"
  • "Bei Kali"
  • "Fitina Yako"
  • "Haraka Haraka"
  • "Mambo Bado"
  • "Ndivyo Sivyo".
Tuzo Walishinda
  • 2003 Tuzo za muziki za lulu la Afrika (Tuzo za PAM) - Msanii wa Mwaka & Msanii bora mwanamme na Msanii bora wa muziki wa Contemporary na Wimbo wa Mwaka ( "Mama Mia") [2] 2004 Tuzo za muziki za lulu la Afrika (Tuzo za PAM) -
  • Msanii wa Mwaka na Wimbo wa Mwaka ( "Jamila") [3]2005 Tuzo za muziki za lulu la Afrika (Tuzo za PAM) -
  • Msanii na Kundi bora wa Afro Beat na Nyimbo bora za Afro Beat ( "Kipepeo") [4]
  • Tuzo za muziki za Tanzania 2004 - Albamu bora ya Afrika Mashariki ( "Bei Kali") [5]
  • Tuzo za muziki za Tanzania 2005 - Albamu bora ya Afrika
  • Mashariki ( "Jamila") [6] 2006 Tuzo za muziki za lulu la Afrika (PAM Awards) -
  • Msanii na kundi bora wa Afro Beat [7]
  • Tuzo za muziki za Kisima 2006 - Nyimbo bora ya Uganda
  • (Mama Rhoda) na video bora ya Uganda (Mama Rhoda)
  • Tuzo za muziki za Kisima 2007 - Nyimbo bora ya Uganda
  • (Sivyo Ndiviyo na Profesa Jay) [9]
  • Ameteuliwa
  • Tuzo za Kora 2003 - Msanii bora wa Afrika Mashariki [7]
  • Tuzo za Kora 2004 - Msanii bora wa kiume wa Afrika
  • Mashariki [10]
  • Tuzo za MOBO 2006 - Tendo bora la Kiafrika [11]
  • 2007 Tuzo za muziki za Ulaya za MTV - Tendo bora la Kiafrika
 
Yuko uganda [emoji1254]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sawa yuko wapi sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yupo mzima wa afya na ana ngoma mpya kali tu,katoa mwezi uliopita kitu safi sana.
Msimfananishe Chameleone na vitu vya kibwege
 
Upo sahihi 100% labda lengo langu ilikiwa ni kumtoa wasiwasi mleta mada ila najua kuwa Jose keshapoteza muelekeo.
 
Hapo kwenye Bifu na Bob whine umenifanya nitakari tofauti iliyo kuwepo kati ya Ray na Kanumba, na kwa sasa Alikiba na Diamond.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ngoma anasikilizia chumbani kwake na mkewe? Hii dunia ni ndogo sana kuwa Muongo ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko kwao bado yupo juu sana kwa taarifa yako huyo legend, pesa na kila kitu yuko fit mtafute utampata na wala hamna ubishi hamna msanii yoyote EA atakuja fanana nae.

Ubishi wa nini nenda youtube utakutana na magoma yake kibao tu ya mwaka jana.
 
Huko kwao bado yupo juu sana kwa taarifa yako huyo legend,pesa na kila kitu yuko fit mtafute utampata na wala hamna ubishi hamna msanii yoyote EA atakuja fanana nae.
Ubishi wa nini nenda youtube utakutana na magoma yake kibao tu ya mwaka jana
Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…