Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,437
- 1,027
Nimepata shuhuda ya barua ya dada mmoja kupitia redio fulani ya kidini.Huyu dada ana watoto watatu,mtoto wa pili kazaa nje ya ndoa,mumewe hajagundua na anampenda mno huyu mtoto wa pili kuliko hata wale wengine wawili ambao ndo wa kwake halali.Huyu dada kaokoka na sasa ni mcha mungu.Kuna kitu kinamweka njiapanda,je..amwambie mumewe ukweli wa yeye kuzaa nje ya ndoa au aifanye siri mpaka kifo chake?Hivi sasa anaishi maisha ya raha mustarehe na mumewe mpenzi,mwanamke ameokoka na anataka kujivua gamba,aanze maisha mapya masafi ya kumpendeza mungu,mpeni ushauri.