Nimepata shuhuda ya barua ya dada mmoja kupitia redio fulani ya kidini.Huyu dada ana watoto watatu,mtoto wa pili kazaa nje ya ndoa,mumewe hajagundua na anampenda mno huyu mtoto wa pili kuliko hata wale wengine wawili ambao ndo wa kwake halali.Huyu dada kaokoka na sasa ni mcha mungu.Kuna kitu kinamweka njiapanda,je..amwambie mumewe ukweli wa yeye kuzaa nje ya ndoa au aifanye siri mpaka kifo chake?Hivi sasa anaishi maisha ya raha mustarehe na mumewe mpenzi,mwanamke ameokoka na anataka kujivua gamba,aanze maisha mapya masafi ya kumpendeza mungu,mpeni ushauri.
Ushauri mzuri S.L,lakini kwa sisi wakristo mtu unatakiwa kutubu,kujuta na kuacha dhambi na baada ya hapo kama ulimkosea mtu,unatakiwa kumfuata kumwomba msamaha ili usamehewe na MUNGU juu mbinguni na wanadamu duniani.Huyu dada ameokoka na kumpokea yesu kristo kama mwokozi wake,anataka kujivua gamba na kuachana na asili chafu ya zamani na kuanza maisha mapya.Mungu anasema maombi ya mtu mwovu ni kelele masikioni mwangu na sadaka ya mtu mwovu ni machukizo mbele ya macho yangu.Kwa hiyo kama akiamua kuficha siri basi aachane na mambo ya uokovu na akae na asili yake ya uovu mpaka kifo chake for the better of her son!Kwa faida ya mtoto simshauri aseme. Atamwathiri huyo mtoto sana. Vile baba mlezi hajagundua,aendelee kubaki na siri yake, afanye maombi na atubu sana, na asirudie tena!
Point taken!Acheni masihara, kwanza huyo mwanamke ni mpumbavu kwanini asingemweleza huyo mwanaume ukweli kabla hawajazama deep katika mapenzi?
Na hakuna siri itakayodumu dunia hii.
Anaonesha kabisa ni mwongo, mnafiki, haina haja yakuokoka. Madhara ya huo ujinga ni makubwa kuliko angesema mwanzo na huyo mwanaume kama anaakili,busara na uelewa wa maisha atamuelewa na wataishi kwa furaha. Rejea filamu ya "THE LOST TWINS" by mtitu game.
Bora mie copy n paste hakuna hata haja ya DNAHuyo mama asirogwe kumwambia mmewe,inahusu? yeye si wa kwanza wala wa mwisho kuzaa nje ya ndoa,mkemia mkuu alisema vipimo vya DNA vimeonyesha 50% ya watoto wanazaliwa na baba chanja,usichokijua ni usiku wa giza na mbwa aliyelala usimwamshe.Maumivu ya kusema 'ukweli' hayataishia kwa baba tu yatahamia kwa mtoto na madhara yake ni mabaya sana,'kitanda hakizai haramu'!