Yussuf ChuChu Afariki Dunia

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2007
Posts
1,407
Reaction score
161
Aliyekuwa mmiliki wa Band ya chuchu sound na Mkurugenzi wa chuchu radio Yusuph Chuchu amefariki dunia jana jijini Nairobi, mazishi yana fanyika leo visiwani Zanzibar. R.I.P Babu chuchu!!


Yusuph Chuchu kushoto.
 
RIP mzee wetu mwenyezi mungu aiweke roho yako pema peponi
Amen
 
RIP babu Chuchu. Hakika kipaji chako kitakumbukwa daima na ulikuwa ni mfano wa kuigwa.
 
 
Yussuf Ahmed Alley AKA Bwan Chuchu amefariki dunia jijini Nairobi-Kenya.

Chuchu alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya mwanzoni mwa 2000 na bendi yake ya Chuchu Sound,iliyokua na wakali kama Mao Santiago,Omary Mkali,Waziri Sonyo,marehemu Gabby Katanga na wengine kibao,hasa na kibwagizo cha ”EEH..KWAHERI” kwenye miondoko ya mduara.

Na mpaka anafariki alikua anamiliki studio ya Heartbeat Records na kituo cha redio cha Chuchu FM vyote vipo kisiwani Zanzibar,na haijajulikana mara moja chanzo cha kifo chake.

Msiba upo Kisima Majongoo na Mazishi yanafanyika kwenye makaburi ya MwanaKwerekwe leo saa 10,kisiwani Zanzibar.

source: mzalendo.net
 
R.I.P Chuchu....yale mambo ya "bwan chuchu konda kantukana..." tutayakosa sana du!
 
rangi ya Madhiiiwa
kweli udongo unameza watu

RIP BWAN CHUCHU
 
RIP, Bwan' CHUCHU........na kama kilivyokuwa kibwagizo chako mwenyewe...EEH? KWAHERII!!
 

Eeh...Kwaheri.R.I.P Bwan chuchu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…