Makamba hapa yuko sahihi, Kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzie hivyo hivyo kwa maskini na maskini. Ukipima maendeleo kimikoa tanzania utaona Kilimanjaro iko juu na kwa kweli chama kilichozaliwa huko kitakua makini zaidi na maendeleo. Sera za Chadema na maneno wanayoongea kwenye kampeni hayana ulinganishi na vyama vingine kwa sababu wanasema kama watu wanaojua na ku experience maendeleo. Sasa wewe mweke Mkwele, atakuambia nini kuhusu maendeleo? kama siyo kukuahidi bajaji za ku mbeba mke wako mjazito mwenye uchungu wa kujifungua? Kwa spidi za bajaji mbali na kuwasababisha maumivu zaidi sijui ni wangapi watakaojifungulia njiani, na ikitokea hivyo sijui itakuwaje maana hamna nafasi ya kutosha kumruhusu kujifungulia ndani, nadhani wataisimamisha bajaji na mke wako atajifungulia pembeni mwa barabara! Hiyo ndiyo tofauti ya maendeleo ya kusikia na kuona, aliyeona maendeleo atatofautisha ambulance na bajaji.