Yutong Vs scania Vs ud

kwenye suala la kuharibika wakati wa safari, yutong hazina guarantee mkuu, afadhali uharibikiwe na skania! Nimewahi kuharibikiwa na basi la Green star kuja mwanza, hapo shinyanga, tulilala hapo hapo! Na kwa taarifa, yutong za green star kuja mwanza zimechoka sana! zinalaza watu njiani mara kibao...wameleta mpya chache ku-backup ila hali sio nzuri, yutong ni janga mzee...hazina maana! zikikorofisha hamuondoki...systems zake ni electrified, haiwezekana kufanya utundu wa kienyeji kama kwa scania.
 
Katika hayo magari kila kitu bora kipo Scania, ila jamaa zako hata akili zao zishakuwa za kichina.
Nasikia kiwanda cha Scania kimechukuliwa na wachina tayari na wanachofanya ni kuendeleza pale wenyewe walipoachia.
 
Yutong speedmeter yake mwisho 140, lakini we njo na speed yako 180 huikamati.
 
Samahani kidogo....na hawa Faw vs Scania kwa upande wa maroli yupi mkali???
 

I think wewe umekuwa mtanzania sana. Mbona umetoa wazi mifano mingi kuonesha ubora wa Yutong as compared to Scania sasa inakuwaje unashindwa kutoa reseach findings zako.
As long as hakuna mtu alio fanya research ubishani wa YOUTONG VS SCANIA stats zake zitakazo letwa hapa itakuwa story za vijiweni tu ambazo aanyeongea sana ndo anashinda.
Unatumbi consumption ya mafuta tupe data authentic sio kwassbu we umeona yutong ulopanda likp hivo basi uka conclude

Eti speed, youtong linakimbia kuliko scania, thst statement is so subjective. Watu waje na stats hapa kuonesha Youtong inakimbia zaidi kuliko scania sio eti kwassbabu superfeo wanatumia Yutong na linawahi kufika Songea kuliko mabasi yanayo tumia scania. Bt mbona Ally's inatumia scania lakini lakini hyo njia ya mwanza, shinyanga hakuna mtu anayeigusa... So based on these subjective reason za mtu moja moja its not ryt to come hapa with that conclusion. This is Jf
 
Mhh???? Hapo kwenye ally's na greenstar. Ile ishu nyingine, naomba tusidanganywe na speed meter, kuna siku nimeifukuzia na corola mpaka 140 bado sikuuikamata . nadhan sisi wenyewe ndo hatujui keundesha biashara zetu Vizuri ila hajanishawishi mtu kununua yutong. za greenstar hazina miaka hata 2. LaKini ukiziangalia huwezi zifananisha na abood au zile za hood kwu uzuri
 
Wazee ila twende mbele turudi nyuma! SCANIA mashine...!
 

kuna mtu anasema ulaya hamna yutong,hii ni nin?
 

Kama mmeweza kubishana, ina maana mnavyo vitu ambavyo kila upande unaamini ndio FACTS.

Labda sasa niwaulize swali, yupo kati yenu hapo kijiweni kwenu ambaye alishawahi kumiliki aina zote mbili angalau aseme kwamba ubishi wake una base kwenye experience?
 
hizi tutong zipo za matumizi ya mjini kama ile ya buffallo na zipo nyingine kwa matumizi ya barabara na mazingira magumu na scania hivyo hivyo .unapotaka kufanya uamuzi wa kununua usivutiwe na muundo ,utaelezwa .pili mafuta .ulaji wa mafuta ni kitu cha kuzinagatia ,engine oil inatumia kiasi gani ,formula iko hivi kama bodi ni nyepesi hutumia mafuta kidogo ,kama bodi ni nzito hutumia mafuta mengi hadi kuchanganya .mfumo wa gea pia huchangia gari kutumia mafuta mengi ,scania ina gea 8-12.yutong model zk3..ina gear 6.injini ni piston 6 ,scania ina piston 8 hivyo uwiano wa mgandamizo hadi kutokea muwako ni mkubwa ,yaani mafuta yanakandamizwa na piston yatatumika mengi .mambo ya transmission haya ni matatizo ya kiufundi yanarekebishika .
 
ile ya buffalo ni ZONDA na sio YUTONG mkuu!
 
Wandugu yutng engine zake ni madhubuti asikudanganye mtu. ni za kimarekani toka magari ya MAN. MBIO NDO NYUMBANI KWAKE HAKUNA CHA MARCOPOLO WALA UD.
we ndugu inaonekana kuwa umetumwa na wachina na hata hoja yako haina mashiko. hebu nenda Iringa panda Yutong halafu mbele yenu ikae scania yeyote au hata nyie mtanglie wakati wa kupanda kitonga halafu uone mziki wa turbo ya scania na ule mluzi wake(turbo) hapo ndio utasema kuwa scania ni noma. acha kudangaya watu lakini. nimepanda new force,green star(zote hizo ni yutong) na hakuna kitu when it comes to Kitonga but scania ooh yeah kama kushuka vile cause pia nimepada scandinavia by then,hood,happy nation na Nganga. wacha kabisa.
 
yutong hawezi kuikamata scania hata siku moja labda km scania imechoka
 
Unapozungumzia ubora na uimara huwezi hata siku moja kulinganisha Scania na Yutong. Scania iko juu kwa kila kitu. Ikumbukwe kuwa kampuni nyingi za kutengeneza magari za China, ikiwa ni pamoja na Yutong, zimeanzishwa hivi karibuni na nyingi zinatumia teknolojia zilizoazimwa aidha Japan au Ulaya. Kwa mfano, haya mabasi ya Yutong (yenye injini mbele) Mchina amechukua teknolojia ya Volvo, hususan iliyotumika kuunda mabasi ya Volvo B7. Hata hiyo, ubora wa mabasi ya Yutong ni wa kiwango cha chini ukilinganisha na Volvo. Kuhusu mbio na uwezo wa kupanda milima, hii inategemea na nguvu ya injini ya basi husika. Injini ya Yutong ina uwezo wa horsepower 260. Ni wazi kwamba Yutong italitimulia vumbi basi la Scania lenye injini yenye uwezo wa horsepower 220, kwa mfano yale mabasi ya Scania F94 ya Hood. Lakini Yutong haiwezi kusogelea Scania F94HB za Abood ambazo injini zake zina uwezo wa horsepower 310. Scania hivi sasa ina modeli ya mabasi ya F330 yenye horsepower 330. Haya yana uwezo wa kuipita Yutong kama imesimama iwe tambarare au kwenye milima. Kama alivyosema mdau mmoja aliyetangulia, moja ya udhaifu mkubwa wa Yutong na ubovu wa ekseli ya nyuma. Wamiliki wengi huondoa ekseli hizo zikiwa bado mpya kabisa na kufunga za Scania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…