Yyuo vya udereva vilivyofungiwa Tanzania

Yyuo vya udereva vilivyofungiwa Tanzania

fungi06

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2020
Posts
738
Reaction score
1,017
Napenda kutanguliza juhudi ya baadhi ya platforms zinazofanya vizuri kutufikishia wanajamii taarifa ambazo ni za muhimu maskioni kwetu...

Nimekua nikifwatilia kwa siku chache sababu zinazo pelekea kuongezeka kwa ajali Tanzani, kumbe kunaanzia mbali sana.

Moja kati ya vyanzo vinavyosababisha ajali kua endelevu nchini kwetu, ni ufwatiliaji mdogo kwenye driving schools zilizopo apa nchi. Ambapo juzi mwaka ukiwa unaanza kuna driving moja mkoani DODOMA nilienda kusomea driving skills, ndio wapo vizuri ila gari ni mbovu (dash board ) haionyeshi kitu kabisa, yani mpaka nikatamani nirudishe pesa yangu sema ndo ivyo basi...

Sasa basi ningependa kuomba kukumbusha kua, driving schools izi pia inabidi zitiwe maanani na serikali sio mnazifungia kutoa lesseni ila mnawaacha wanaaendelea kufundisha.

Huku nikupoteza mda na pesa, kwanini wasifungiwe vyote mpaka wakae sawa kwa ajili yakutoa huduma?

Alafu kwanini isieleweke tu kua vyuo vya udereva ni VETA NA NIT ivi vingine vinafungiwa mda wowote!

Hapo kwenye taarifa mmetoa idadi tu kua "vyuo 161 vimefungiwa!", ila hamna maali inaonyesha LIST YA VYUO HIVYO vilivyofungiwa?

Mwenye list ya vyuo hivyo atuwekee, ili watu wengine wanaotaka kwenda driving now, wasichome pesa zao.

Tokomeza wachoma pesa zetu mitaani.

#Tanzania bila scammers inawezekena.

=====

Jeshi la Polisi Tanzania limesema Shule/Vyuo 161 vimefungiwa kutoa mafunzo ya udereva kwa kuwa havijakidhi sifa na vigezo hii ni kufuatia ukaguzi ambao ulifanywa kwa agizo la IGP Camilius Wambura kama sehemu ya kudhibiti wimbi la ajali.

“Zoezi la uhakiki lilianza January 02,2023, Shule/ Vyuo vilivyohakikiwa ni 297 na vyenye sifa ni 134”

“Umefanyika pia ukaguzi wa leseni 20,944 ambazo zimehakikiwa ambazo ni sawa na 1.3%, kati ya hizo leseni 17,726 za Madereva zimebainika kuwa na sifa na wamepewa barua ya udhibitisho”

“Leseni 3,214 za Madereva zimefutiwa madaraja kwani madereva wa leseni hizo hawana sifa ya kuwa na madaraja C na E kutokana na sababu za kutosomea madaraja stahiki”
 
Vyuo vya elimu mkifungia list inakua attached, ila list ya vyuo vya udereva ndo kile cha mfuko wa vifo vya maaskari,,

Wanaotulinda nchini kwetu ndo wanaoongoza kula pesa chafu
 
Dah! Mimi nimesoma driving schools kwa mfumo wa nadharia tu, tena kwa siku chache! Halafu baadaye nikakabidhiwa cheti changu cha uongo na kweli.

Maana mpaka naenda kujiandikisha, tayari nilikuwa dereva nisiye na leseni kwa miaka 8! Na hapo nilijifunzia kwenye gari yenye manual gear box. Nakumbuka nilichofaidika kwenye yale mafunzo, ni alama chache tu za usalama barabarani ambazo nilikuwa sizielewi hapo kabla.
 
Dah! Mimi nimesoma driving schools kwa mfumo wa nadharia tu, tena kwa siku chache! Halafu baadaye nikakabidhiwa cheti changu cha uongo na kweli.

Maana mpaka naenda kujiandikisha, tayari nilikuwa dereva nisiye na leseni kwa miaka 8! Na hapo nilijifunzia kwenye gari yenye manual gear box. Nakumbuka nilichofaidika kwenye yale mafunzo, ni alama chache tu za usalama barabarani ambazo nilikuwa sizielewi hapo kabla.
Lesen ushapata
 
Miaka mingi imeshapita. Na ndiyo lilikuwa lengo hasa la kulipia hayo mafunzo. Walituahidi kutoa leseni baada ya kupata vyeti.
Wanazingua mno hii sekta imekaa kihuni ndo maana ajali aziishi
 
Unakutana na jamaa wa TRA bar, tena kwenye viti virefu, anakuambia njoo na kiasi fulani cha pesa upate leseni. Huyu aliyepata leseni chuo chake ni kipi?
 
Back
Top Bottom