Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Wewe Mzee wa kijijini
Kula zabibu umeanza lini
Waachie watu wa mjini
Zabibu iwe mwao akilini
Balantanda usimzalau mzee wa kijijini ooh! shauri yako
anyways i am otu for the day!....see you all manyana...i got go cook for my cupcake.you know how it is inabidi na mimi nipalilie shamba langu maana mimi ni tunda uwii!...
xoxo
I know... didn't I say I'm a first learner too?
Zabibu ukijapewa
Hilo utalichukuwa
La bure ukimegewa
Utalila kama muwa?
Vipi kama bado bichi,
Tena kijani kibichi,
Utatusa kuwa mbichi
Au hata hivyo huliachi?
Vipi ukilingishiwa,
Kinywani kupitishiwa
Ulimini kuonyeshwa
Kisha likaondolewa?
Haiba yake machoni
Furaha tele moyoni
Toka ganda hadi ndani
Livutie utamani
Hizo ndogo mdomoni
Zaishilia kooni
Hilo nalo na shinani
Sitamani muwashani
Langu laja kwa mafungu
Uchaguzi ni wa kwangu
Nabeba wote mkungu
Hadi kunako uvungu
Sijali zielemee
Siziachi zilegee
Watu,ndege hata mee
Siwachi wasodolee
...kimya kimya...
jamani tunda nanasi
kula uwe na nafasi
unapojaa ukwasi
hautajifaidia
kwa chakula cha mchana
mezani kimejazana
juisi yake mwanana
hakika utasifia
nanasi liwe shinani
wachuma kiulaini
hakuna purukushani
mkononi wachukua
Embe dodo kule juu
hadi lidondoke puu!
kweli kwa mtaji huu
hupaswi kulisifia
jamani hizo zabibu
hasa alolima babu
sana sana kwa ulabu
kama wataka kulewa
nakukaribisha kwangu
leo maulidi yangu
ule nanasi mwanangu
ni tamu tena murua
Wewe kula hizo ndizi,
Wengine wala andazi,
Hata ule tangawizi,
Zabibu tunda la kazi!
Hadi umenye maganda,
yale yalogandaganda,
Ndiyo ule lako tunda,
Hilo unalolipenda.
Uzuri wake zabibu,
Kula kwake siyo tabu,
Mdomoni taratibu,
Nafyonza kama tabibu.
Ndizi ina ukakasi,
Ulimini kama pasi,
Zabibu ladha halisi,
Mwenyewe najinafasi!
Mundu kasema nanasi,
Kwangu halina nafasi,
Zabibu siwezi asi,
Nisije jipa mkosi!
Zabibu ninalo hamu,
Mengine siyo matamu,
Nitalila kitaalamu,
Kama nilivyo mwalimu!
Njoo uje huku kwa energy needs bana.
Tusiishie tunda tunda...huku mabazazi wanakata mti.
duh.. wapi tena usije kukuta mti wa tunda wenyewe umekatwa!!
Being slow.
Huku kwa DOWANS silly.
Mimi nina swali moja
Mara kichwani huja
Sitegemei vioja
Bali jibu lenye hoja
Mimi nataka kujua
Linahisije kuliwa
Tunda linalosifiwa
Au halina hisia?
Zabibu, nanasi, embe
Hivyo vyote ni viumbe
Vipi navyo visitambe
Atambe mshika jembe?
Mwenye ujuzi fumbua
Linahisije kuliwa
Tunda mnalochukua
Ganda lake kulivua?
Wewe kula hizo ndizi,
Wengine wala andazi,
Hata ule tangawizi,
Zabibu tunda la kazi!
Hadi umenye maganda,
yale yalogandaganda,
Ndiyo ule lako tunda,
Hilo unalolipenda.
Uzuri wake zabibu,
Kula kwake siyo tabu,
Mdomoni taratibu,
Nafyonza kama tabibu.
Ndizi ina ukakasi,
Ulimini kama pasi,
Zabibu ladha halisi,
Mwenyewe najinafasi!
Mundu kasema nanasi,
Kwangu halina nafasi,
Zabibu siwezi asi,
Nisije jipa mkosi!
Zabibu ninalo hamu,
Mengine siyo matamu,
Nitalila kitaalamu,
Kama nilivyo mwalimu!
Ni tamu hilo la kwangu,
Nafyonza kivyanguvyangu,
Ni tamu kuliko Changu
Nimelirundika chungu!
Siyo tunda la kizungu,
La Uru siyo Marangu,
Nalamba vidole vyangu,
Naruka kama kulungu!
... litaendelea...
Swali lako ni makini
Ila ndani ni mtego
Umetegwa kilaini
kunasa wenye magego!
Siri nitaifichua
Hisia zake matunda,
Hili ukishalijua
Na mti utaupanda!
Tunda lapenda kuliwa,
Linapenda kutafunwa,
Langoja kutunguliwa,
Pole pole likamenywa!
Kisu kikapenya kati,
Mchuzi ukamwagika,
Bila hata varangati,
Meza tukaziandika.
Ndiyo maana yaiva,
Ili baadaye yaliwe,
Mengine yasiyoiva,
Kwanini yatunguliwe?
Raha yake ni kung'atwa
Au kisu kuchomekwa,
Na kisha hata kupikwa,
Jikoni yakabandikwa!
Yanajitoa mhanga,
Matunda nayasifia
Na yale yanayoringa,
Watu wanayachukia!
Raha ya tunda kuliwa
Mbinguni wameandika
Na mbegu zapunjuliwa
Wa kijiji naandika.
Kalamu naweka chini,
Tunda langu limeiva,
Kisu kiko mkononi
Tunda kalileta Eva!!