Zabron singers kwenye sherehe za kumuapisha Ruto

BRN

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
5,188
Reaction score
6,633
Hawa jamaa jana tarehe 13/09/2022 kwenye sherehe za kumuapisha Rais mteule wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Kenya Mhe.Ruto walifanya makubwa sana walipowainua na kuwachezesha maelfu kwa mamia ya Wakenya pale Kasarani.

Hakika mmetuwakilisha vema..huu wimbo wao wa Nimeuona Mkono wa Bwana hakika una ujumbe murua sana.
Kongole kwao japo Wakenya hawakawii kusema hawa waimbaji ni wakwao maana wao kila kitu kizuri ni cha kwao.
 
Ruto ni wimbo wake/kwaya yake pendwa hiyo...kwenye kampeni hata kabla ya kampeni ameucheza na kuimba sana huo wimbo....

Nilijua tu lazima wangeitwa Kasarani....
Utakuwa unamaanisha mengi sana kwenye maisha yake.
 
Pongezi nyingi kwao.
Wengine wnapenda kuwaalika wale wakata mauno, wanaimba mambo hata hayaeleweki
Kwenye kmpn wanawambia watu rusha mikono juu ,sijui sema oyoooo
Mara inamaa nkuchomeke gdmit

Ova
 
Raila Odinga alichemka pakubwa sana kumualika Diamond siku ya kufunga kampeni zake za Urais!

Ukijumlisha na mamilioni ya shilingi aliyolipwa, hakika Wakenya wengi walighadhabika. Maana waliona kama wamedharauliwa vile!
 
Watanzania nyie mna wasanii wengi Sana mbona msitugawe hao Zabron singers na sisi tujivunue.

Mwanzo Nilikuwa najua Hawa majamaa Ni wa kwetu kumbe Ni wa huko Tz eti🤔
 
Reactions: BRN
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…