El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 297
- 537
Nianze kwa kukiri kwamba nilifurahishwa kiasi kumuona Halima akitueleza vile mama yake alivyompa neno la faraja kutoka kitabu cha zaburi 35 katika masaibu yake.
Ni tabia njema upande m moja kuona Watu wanakimbilia msaada wa vitabu vitakatifu kwa ajili ya faraja au hata kupata ufumbuzi wa shida zao. Hapa nampongeza Halima kwa kukumbuka maandiko.
Tatizo tu ninaloliona ni kama hiyo zaburi inaendana na matatizo yake ya sasa.
Kwa sisi ambao kiasi tunafuatilia mafundisho ya kidini, mara zote huwambiwa kwamba" maandiko huwa yana asili yake na aina yake ya kutafsiri. Alichofanya Halima ingawa kanukuu maandiko lakini yako nje ya maana(out of context).
Mtunga zaburi anaposema Mungu apigane na wanaopigana naye, hana maana Mungu apigane vyovyote(blindly) bali mtunga zaburi hapo, kama mtu mwenye haki (Righteous) anataka Mungu awe upande wake!
Kumbuka Mungu huwa upande na wenye haki.
Je, wakati Halima anajifariji kwa hiyo zaburi, ni kweli roho yake inamshuhudia kuwa mwenye haki ktk sakata lake? Maana kujifariji kwa maandiko wakati roho yako inakushuhudia vinginevyo ni faraja hewa.
Nakubaliana na alichosema mchungaji Msigwa mahali fulani kwamba, Halima na wenzake wanapaswa kutubu maana " dhambi iliyotubiwa haina nguvu tena" badala ya kujifariji kwa maandiko.
Ni vizuri kujifariji kwa maandiko lakini in right motive and not in wrong motive.
Utapata amani sana Halima na wenzako endapo utatubu ulivyofanya kinyume na order na taratibu zenu badala ya kupata faraja ya maandiko ambayo hayakutii moyo kuishi bila order. Kujifariji kwa maandiko wakati mzizi wa dhambi umefichwa ni kutafuta amani ya bandia ambayo haitakusaidia kwa hakika.
Wasalaam.